Pages

Monday, December 10, 2012

FRANCIS MIYEYUSHO AKATA KILIMILIMI CHA NASSIBU RAMADHAN KWA KO



BONDIA Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ amefanikiwa kutetea taji lake la WBF uzito wa Bantam, baada ya kumpiga Nassib Ramadhan kwa Techinical Knockout (TKO) raundi ya 10 kwenye ukumbi wa PTA, Saba Saba, Temeke mjini Dar es Salaam jana usiku.

Nassib ambaye mwanzoni alioneka kuzimudu ngumi kwani alimrushia mpinzani wake makonde mazito yaliyomyumbisha lakini alianza kuishiwa pumzi raundi ya nane, lakini alijikongoja kutaka kumaliza raundi 12 za pambano hilo, ila safari ikaishia raundi ya 10.

Nasib aliendelea kutawala pambano hadi raundi ya sita, ila baada ya hapo, mwelekeo wa pambano ulianza kubadilika taratibu, ndipo Chichi, Mtoto wa Kinondoni akianza kumuadhibu mpinzani wake kwa makonde yake yaliyoshiba uzito.

Baada ya kuona amezidiwa Nassib alitumia ujanja wa kumkumbatia Miyeyusho ili kumpunguza kasi.

Kwa matokeo hayo Francis Miyeyusho aliondoka na mikanda miwili na kutangazwa kuwa bondia bora wa mwaka na chama cha Ngumi za kulipwa (TPBO)

Katika mapambano ya awali, Deo Samuel alitoka sare na Freddy Sayuni, Mohamed Matumla alimpiga kwa Knockout (KO) raundi ya pili Deo Miyeyusho,  na Ibrahim Classic alimpiga kwa pointi mbili kwa moja Said Mbugi na Fadhil Majiha alimpiga kwa pointi mbili kwa moja Juma Fundi na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa UBO

Mgeni rasmi, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, awali wakati akifungua pambano hilo aliwataka mabondia na viongozi kuwa na nidhamu katika kuendeleza mchezo huo kwani ni sehemu ya ajira.

"Serikali kali yetu inataka michezo yote iwe bna mashabiki kama soka hivyo viongozi na mabondia mnapaswa kuwa na nidhamu kwani michezo ni ajira", alisema Fenella

Baada ya pambano hilo lililohudhuriwa na maelfu ya mashabiki kumalizika Waziri Fenella alimvisha bondia Francis Miyeyusho wake.

No comments:

Post a Comment