Pages

Saturday, December 8, 2012

MAKUNDI NA RATIBA YA UHAI CUP HANDARANI

SHIRIKISHO la soka nchini leo limetoa ratiba na makundi ya timu zitakazo shiriki mashindano ya Uhai yanayodhaminiwa na Bharessa Group of Company kupitia bidhaa yake ya maji ya uhai.

Draw hiyo imechezeshwa leo kwenye ofisi za TFF mbele ya waandishi wa habari na wawakilishi wa vilabu na ilisimamiwa na Salum Madadi ambaye ni Afisa maendeleo ya Soka wa shirikisho la Soka nchini.

Mashindano haya yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 11 mwaka huu, jijini Dar es salaam na yatashirikisha timu 14 ambazo zimegawanywa kwenye makundi matatu kwenye viwanja vya Azam Complex Chamazi na Karume.

Kundi A na Kundi B litakuwa na timu tano tano ambapo yatatoa timu tatu zitakazoingia robo fainali na kundi C litatoa timu 2 zitakazoingia robo fainali.

Jumla ya timu 8 zitaingia robo fainali ambayo itachezwa tarehe 18 na 19 Desemba, nusu fainali itachezwa Desemba 21 na fainali ni Desemba 23.

Kundi A lina timu za
 Coastal Union
Tanzania Prison
JKT Ruvu
Mtibwa Sugar
Toto African

Kundi B
African Lyon
Polisi Moro
Azam FC
JKT Mgambo
Simba SC

KUNDI C
Kagera Sugar
JKT Oljoro
Yanga
Ruvu Shooting

RATIBA YA KUNDI A                           RATIBA KUNDI B                        RATIBA KUNDI  C
Coastal Union vs Tanzania Prison           African Lyon vs Polisi Moro        Kagera Sugar vs JKT Oljoro
JKT Ruvu  vs Mtibwa                           Azam vs JKT Mgambo               Yanga SC vs Ruvu Shooting
Toto African vs Coastal Union               Simba SC vs African Lyon          JKT Oljoro vs Yanga SC
JKT Ruvu vs Tanzania Prison                Azam vs Polisi Moro                   Ruvu Shooting vs Kagera Sugar
Mtibwa Sugar vs Toto African               JKT Mgambo vs Simba SC        Kagera Sugar vs Yanga SC
Coastal Union vs JKT Ruvu                  African Lyon vs Azam                JKT Mgambo vs Ruvu Shooting
Tanzania Prison vs Mtibwa                    Polisi Moro vs JKT Mgambo
Toto African vs JKT Ruvu                     Simba vs Azam
Mtibwa Sugar vs Coastal Union             JKT Mgambo vs African Lyon
Tanzania Prison vs Toto African              Polisi Moro vs Simba

Mwandishi wa Habai akiokota karatasi zenye jina la timu na kingine chenye kundi kwenye visanduku vilivyowekwa mezani tayari kwa upangaji wa makundi





No comments:

Post a Comment