Pages

Monday, December 10, 2012

KIM ATANGAZA JESHI LAKE, AWATEMA MESI NA EDWARD CHRISTOPHER, AWALETA HAMIS MCHA

Kuelekea katika mchezo wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa Zambia maarufu kama Chipolopolo mchezo ambao umepangwa kufanyika tarehe 22/12/2012 katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Kim Poulsen ametangaza kikosi chake.
Katika kikosi hicho Poulsen amewaita baadhi ya wachezaji kwa mara ya kwanza akiwemo mlinda mlango Aisha Manua wa kikosi cha pili cha Azam, Samir Nuhu na Hamisi Mcha Hamisi wa Azam ambao walifanya vizuri katika kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar iliyoshika nafasi ya tatu katika michuano ya chalenji mjini Kampala, Uganda.
Poulsen amewapunguza wachezaji wawili vijana wa klabu ya Simba Edward Christopher na Ramadhani Singano na mlinda mlango wa Azam Deo Munish 'Dida'.
Kocha huyo pia amemrudisha katika sehemu ya ulinzi kitasa wa Yanga Nadir Haroub 'Kanavaro' 
Kikosi kamili kilichotangazwa na Poulsen amewaita walinda mlango Juma Kaseja, Mwadin Alli ya Aishi Manua.
Walinzi ni Shomari Kapombe, Nassoro Masudi Cholo, Samir Nuhu, Erasto Nyoni, Issa Rashidi, Aggrey Moris, Amir Maftaha na Kelvin Yondani.
Viungo ni Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Salum 'Abubakar sureboy', Mbwana Samatta, Athumani Iddi 'Chuji' , Amri Kiemba, Hamisi Mcha Hamisi na Shabani Nditi.
Washambuliaji ni John Bocco, Simon Msuva, Mwinyi Kazimoto, na Thomas Ulimwengu.
Baada ya mchezo dhidi ya Zambia tarehe 22/ 12/ 2012, timu hiyo itarejea tena kambini Januari 6 mpaka 20 ikiwa na wachejaji 18 kwa ajili ya michezo ya kujipima nguvu na timu tatu ambazo kocha Kim Poulsen ametaka atafutiwe timu zitakazo shiriki michuano ya wachezaji wa ndani ( CHAN )

Stars inakabiliwa na michezo kadhaa ya kuwania kucheza kombe la dunia ambapo mwezi March itakuwa na kibaru cha awali dhidi ya Morrroco kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa mwezi June.
Mwezi huo huo itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Ivory Coast kuwania kucheza kombe la dunia lakini pia kutakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Uganda wa kuwani kufuzu fainali za mataifa ya Afrika UGANDA

No comments:

Post a Comment