Kuelekea
katika mchezo wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa Zambia maarufu kama
Chipolopolo mchezo ambao umepangwa kufanyika tarehe 22/12/2012 katika
uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, kocha mkuu wa timu ya taifa ya
Tanzania Kim Poulsen ametangaza kikosi chake.
Katika kikosi hicho Poulsen amewaita baadhi ya wachezaji kwa
mara ya kwanza akiwemo mlinda mlango Aisha Manua wa kikosi cha pili cha
Azam, Samir Nuhu na Hamisi Mcha Hamisi wa Azam ambao walifanya vizuri
katika kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar iliyoshika nafasi ya tatu
katika michuano ya chalenji mjini Kampala, Uganda.
Poulsen
amewapunguza wachezaji wawili vijana wa klabu ya Simba Edward
Christopher na Ramadhani Singano na mlinda mlango wa Azam Deo Munish
'Dida'.
Kocha huyo pia amemrudisha katika sehemu ya ulinzi kitasa wa Yanga Nadir Haroub 'Kanavaro'
Kikosi kamili kilichotangazwa na Poulsen amewaita walinda mlango Juma Kaseja, Mwadin Alli ya Aishi Manua.
Walinzi ni Shomari Kapombe, Nassoro Masudi Cholo, Samir Nuhu, Erasto Nyoni, Issa Rashidi, Aggrey Moris, Amir Maftaha na Kelvin Yondani.
Viungo
ni Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Salum 'Abubakar sureboy', Mbwana
Samatta, Athumani Iddi 'Chuji' , Amri Kiemba, Hamisi Mcha Hamisi na
Shabani Nditi.
Washambuliaji ni John Bocco, Simon Msuva, Mwinyi Kazimoto, na Thomas Ulimwengu.
Baada ya mchezo dhidi ya Zambia tarehe 22/ 12/ 2012, timu hiyo itarejea
tena kambini Januari 6 mpaka 20 ikiwa na wachejaji 18 kwa ajili ya
michezo ya kujipima nguvu na timu tatu ambazo kocha Kim Poulsen ametaka
atafutiwe timu zitakazo shiriki michuano ya wachezaji wa ndani ( CHAN )
Stars
inakabiliwa na michezo kadhaa ya kuwania kucheza kombe la dunia ambapo
mwezi March itakuwa na kibaru cha awali dhidi ya Morrroco kabla ya
mchezo wa marudiano utakaochezwa mwezi June.
Mwezi
huo huo itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Ivory Coast kuwania kucheza
kombe la dunia lakini pia kutakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Uganda
wa kuwani kufuzu fainali za mataifa ya Afrika UGANDA
No comments:
Post a Comment