Pages

Wednesday, December 19, 2012

HARUNA MOSHI "BOBAN" AANZA MAZOEZI TENA NA SIMBA




KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban,’ leo ameanza mazoezi rasmi katika kikosi cha timu hiyo, kinachojiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Boban aliungana na wachezaji wenzake katika mazoezi yaliyofanyika Ufukwe wa Coco Beach, Dar es Salaam, yaliyosimamiwa na Meneja wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.

Kiungo huyo alisimamishwa na Kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo, kutokana na madai ya utovu wa nidhamu, baada ya mchezo wao dhidi ya Mgambo Shooting, uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Boban amerejea kimya kimya kwenye kikosi hicho, baada ya suala lake kumalizwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Rage.
Hata hivyo, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga, alipoulizwa leo, kuhusu kurejea kwa kiungo huyo, alisema hajui lolote, ingawa suala hilo lilikuwa chini ya mwenyekiti wake.

Boban alisimamishwa siku 21 na kutakiwa kuandika barua ya kujieleza kabla ya kuchukuliwa hatua nyingine

No comments:

Post a Comment