Pages

Wednesday, December 19, 2012

TANZANIA YAPAA NAFASI NNE VIWANGO VYA UBORA FIFA



TANZANIA imepanda nafasi nne kutoka 134 hadi 130 kwenye orodha ya viwango bora vya soka vilivyotolewa jana na Shirikisho la Soka Kimataifa (FIFA) huku wakiwa nafasi ya 38 miongoni mwa nchi za Afrika.

Mwezi uliopita, Taifa Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Tanzania kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro, ilicheza mchezo moja wa kimataifa wa kirafiki kwa mujibu wa kalenda ya FIFA.

Taifa Stars ilicheza na Harambee Stars ya Kenya katika Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na beki wa kati Aggrey Moris.

Uganda ambao walifanikiwa kutetea ubingwa wa michuano ya Chalenji mwezi huu ikiwa ni ushindi wao wa 13, wanafunga mwaka wakiwa miongoni mwa nchi 100 bora.

Mabingwa hao wa CECAFA ambao wamepanda nafasi mbili wapo katika nafasi ya 84 ambapo Afrika wapo nafasi ya 22 wakifwatiwa na Sudan ambao wamepanda nafasi moja hadi 101.

Burundi ndiyo taifa lililofanya vyema ambapo imepanda nafasi 24 na kumaliza mwaka ikiwa nafasi ya 104 kimataifa na 27 Afrika huku wawakilishi pekee wa CECAFA michuano ya Kombe la Afrika mwezi ujao, Ethiopia ikishika nafasi ya 110 baada ya kushuka nafasi nane.

Kenya imeshuka nafasi nne na kumaliza mwaka ikiwa nafasi ya 134, huku Rwanda pia ikiwa nafasi ya 134 baada ya kushuka nafasi 12 ikifuatiwa na Somalia ambao imeshuka nafasi mbili na kushika nafasi ya 195. Eritrea ni ya 196 baada ya kushuka nafasi nne, Sudan Kusini ni ya 199 na Djibouti ipo nafasi ya 202.

Kimataifa Hispania ndiyo inaongoza kwa ubora duniani ikifuatiwa na Ujerumani na Argentina wakati nchi tatu za juu Afrika ni Ivory Coast, Algeria na Mali.

No comments:

Post a Comment