Pages

Thursday, December 20, 2012

Hansen anavyomtabiria Agger kuibeba Liverpool

NI jambo la kawaida kwa kila mwanadamu kuwa na ndoto zake kuhusu jambo fulani  analoliwaza akilini mwake.

Wapo wanaowaza kujenga majumba ya kifahari wakati hali zao zikiwa duni,wapo wanaowatabiria wenzao kufanya makubwa  huku wakifahamu fika hawawezi kufanya jambo hilo wanalowatabiria.

Na hii ndivyo inavyoweza kuwa kwa mchezaji wa zamani wa timu ya Liverpool, Alan Hansen ambaye kwa mawazo yake anaona kuwa mchezaji Daniel Agger anaweza kuiongoza timu hiyo hadi ikatwaa ubingwa Kombe la Ligi ya Europa.

Hansen, ambaye amewahi kutwaa ubingwa wa Kombe hilo la Ulaya mara tatu akiwa na timu hiyo ya Liverpool anaamini kuwa beki huyo wa kushoto ana kila aina ya  kiwango ambacho kinaweza kumfanya awe beki bora katika klabu hiyo.

Liverpool jana ilikuwa ikisubiri kwa hamu  kufahamu ni timu gani itakutana nayo katika hatua ya  32 ya mashindano hayo baada ya kuchezeshwa  droo   ya kupanga timu iliyokuwa ikichezeshwa jana mjini   Nyon, Uswizi.

Hata hivyo  Hansen  anasema kuwa anavyoamini beki huyo Mdenmark  mwenye umri wa miaka   28,  na mchezaji mwenzake  Martin Skrtel, wataelewana na kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa.

Mscotland huyo anasema: “Ukiangalia katika sehemu ya beki wa kati  Liverpool  ipo fiti  na  Daniel ni mmoja wapo wa wachezaji wanaoimarisha sehemu hiyo,"

Anasema kuwa mchezaji huyo anaimiliki vilivyo sehemu hiyo  na kwamba  unapoangalia kati ya mabeki  10  bora  na yeye yumo.

Mchezaji huyo wa zamani anasema  licha ya mchezaj huyo kucheza katika nafasi ya beki wa kati,  lakini amekuwa akipanda  na kushuka jambo ambalo linamfanya aelewane vizuri  na  Skrtel  na anasema kuwa kila mmoja anaelewana vizuri na mwenzake.

“Skrtel ana nguvu na   Daniel  ni bora uwanjani,”anasema.


Pamoja na kuwa kwa sasa Liverpool  inashika nafasi ya   12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu,  mkongwe  anasema kuwa kocha wa timu hiyo kwa sasa anahitaji msaada wa kuiwezesha timu hiyo kupata ushindi  katika mzunguko wa Ligi Kuu.

Hansen ambaye liigharimu  Liverpool  pauni  110,000  wakati akijiunga nayo mechi yake ya kwanza  ya Ligi Kuu ambayo ilipigwa kwenye uwanja wa Anfield ilikuwa ni  Septemba  24, 1977  dhidi ya timu ya  Derby County ambapo wageni hao walifungwa bao 1-0  lililofungwa   na mchezaji  Terry McDermott.

Bao  la kwanza kwa Hansen lilipatikana mwezi uliofuata wakati wa mechi Kombe la Ulaya mzunguko wa  pili iliyopigwa Oktoba 19 ,1977, katika mechi hiyo ya kwanza iliyopigwa tena kwenye uwanja huo wa Anfield kinara huyo ndiye aliyezikitikisa nyavu akiwa wa kwanza dakika ya 14 ya mchezo huo ambao   Liverpool  iliiadhibu timu kutoka nchi iliyokuwa Ujerumani Mashariki,  Dynamo Dresden  mabao  5–1.

Na tangu kipindi hicho Hansen alikuwa  akipangwa kikosi cha kwanza  hadi anaodoka mwaka  1991 akiwa ameichezea timu hiyo mechi
434

Kwa sasa mkongwe huyo ameteuliwa kumsaidia kocha wa sasa wa timu katika kutafuta wachezaji wa kusajili wakati dirisha dogo litakapofunguliwa mapema Januari mwakani.

No comments:

Post a Comment