FAMILIA ya mwanasoka David Beckham ametawazwa kuwa familia bora duniani kwa utanashati kuliko familia yoyote kwa watu mashuhuri.
Kwa ushindi huo wa asilimia 29 nyota hao watakuwa wamewapiku wapinzani wa nchini Marekani familia ya akina Kardashian na Jolie-Pitts ambao walikuwa wakishikilia taji hilo.
Katika kura hizo dada zake Kardashian wanashika nafasi ya pili wakiwa na asilimia 14 na hivyo kuwapiku Brad Pitt na Angelina Jolie ambao wanashika nafasi ya tatu kwa umalidadi huku mtoto wa Beyonce, Jay-Z aitwaye, Blue Ivy akishika nafasi ya nne.
No comments:
Post a Comment