Pages

Monday, December 24, 2012

CHEKA NA MMALAWI CHIMWEMWE WATAMBIANA

Mabondia Cheka na Chimwemwe wakiwa na promota Andrew George wakiwa wameshikila mkanda wanaogombea

Bondia Francis Cheka

Bondia Chiotcha Chimwemwe toka Malawi

Wanamuziki wa nakotonako

MABONDIA Francis Cheka na Chiokta Chimwemwe toka Malawi wametambiana kuonyeshana kazi kwenye pambano lao litakalochezwa  siku ya boxing day la raundi 12 ubingwa wa IBF  kwenye uwanja wa Sheikh Abeid Amani Karume jijini Arusha.

Wakizungumza kwenye kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Ngorongoro, Naura Spring hoteli, Arusha, mabondia hao wamesema watahakikisha kuwapa burudani mashabiki wa Arusha na vitongoji vyake.


Naye Promota wa pambano hilo alisema kuwa taratibu zote zimekamilika na mabondia watapima uzito kesho .
 "Taratibu zote za pambano zimekamilika kilichobaki nawaomba mashabiki wa ngumi kuja kwa wingi kupata burudani ya ukweli", alisema George

Pia George alisema anaamini watu wa Arusha wanapenda ngumi na siku hiyo ni siku ya sikukuu hivyo watakuja kwa wingi pamoja na familia zao kwani pambano litaanza saa nane mchana.

Pia alisema mabondia watapima uzito siku leo kwenye hoteli ya Naura Spring.

Pambano hili litakuwa ni la raundi 12 na kutakuwepo na mapambano ya utangulizi wa mabondia 11, saba yakiwa ya mabondia chipukizi ya raundi nne kila moja.

Pia ulinzi utakuwepo wa kutosha, alisema George  na viingilio ni shilingi 20,000, 10,000 na watoto 5000

No comments:

Post a Comment