SIMBA YAPATA NAFASI YA TATU
Simba
imetwaa nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha
timu zenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada
ya kuitandika Mtibwa Sugar ya Morogoro mabao 3-0.
Hadi
mapumziko katika mechi hiyo iliyochezwa leo asubuhi (Desemba 23 mwaka
huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam, Simba ilikuwa
mbele kwa bao 1-0.
Mabao
yote ya washindi katika mechi hiyo yalifungwa na Ramadhan Mkipalamoto.
Mfungaji alifunga bao la kwanza dakika ya 43 wakati mengine alipachika
dakika za 57 na 70. Kwa kunyakua nafasi ya tatu, Simba imeondoka na
kitita cha sh. 500,000.
Rambadhani Mkipalamoto ndiye aliyeibuka mfungaji bora wa mashindano hayo.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah akimkabidhi zawadi ya
mfungaji bora wa mashindano ya vijana chini ya miaka 20 ya Uhai Cup, Ramadhani
Mkipalamoto wakati wa fainali ya michuano hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa
Karume jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment