Pages

Sunday, November 25, 2012

VILLA SQUAD YAMALIZA MZUNGUKO WA KWANZA KWA USHINDI MWEMBAMBA



TIMU ya Villa Squad jana  iliifunga Green Warriors bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Karume jijini Dar es salaam

Mchezo huo ambao ulikuwa wa ushindani kiutokana na timu zote kushambuliana kwa zamu ulishuhudia timu zote zikienda mapumziko bila kufungana.


Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko lakini Villa Squad ndio waliobahatika baada ya mshambuliaji wao Juma Juma kufunga bao kwa shuti la mbali.

Green Warriors watajutia mchezo huo kutokana na washambuliaji wake kutokuwa makini kwani walikosa mabao ya wazi mara kadhaa.

Kocha wa Green Warriors alilalamikia mwamuzi wa mchezo huo kwa kutochezesha kwa kufuata sheria.

"Mwamuzi hakututendea haki kutokana na kwamba tunachezewa faulo halafu tunaadhibiwa sisi na si mara yake ya kwanza kutufanyia hivi hata mchezo na Moro United alitufanyia hivi", alisema kocha Salum Dialo.

Naye kocha wa Villa Squad Bakari Idd aliwasifu wachezaji wake kwa kucheza vizuri japo alisema bado washambuliaji hawako makini wanapolikaribia lango la wapinzani.

No comments:

Post a Comment