Pages

Saturday, November 17, 2012

UCHAGUZI WA TFF SASA KUFANYIKA MWAKANI

Uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) unatarajiwa kufanyika Februari, mwakani.

Akitangaza uchaguzi huo Mwenyekiti wa kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji, Alex Mgongolwa amesema uchaguzi huo umesogozwa mbele ili kupisha marekebisho ya katiba ya TFF kama walivyoagizwa na Shirikisho la Soka barani Afrika. (CAF)

Kipengele kinachotakiwa kuingizwa kinahusu “Club Lincencing” kama ilivyoagizwa na CAF katika waraka wake unaowataka wanachama wote wa CAF kuingiza kwenye katiba zao.
   
Mngongolwa alisema kutokana na ushauri na maagizo ya FIFA, TFF inatakiwa kuunda wa Kamati ya Rufaa ya Uchanguzi (“Elections Appeals Committee”) na kuondokana na utaratibu tulionao hivi sasa ambao Kamati ya Rufaa (“Appeals Committee”) inajigeuza na kuwa Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi wakati wa mchakato wa uchaguzi wa TFF.
  
Pia kuindoa nafasi ya Makamu wa Pili wa TFF pamoja na kutamka kuwa Wawakilishi wa klabu za Ligi Kuu katika Kamati ya Utendaji watachaguliwa moja kwa moja na klabu zenyewe.

Pia azimio la Mkutano Mkuu uliopita la kuruhusu uundwaji wa chombo huru cha kusimamia Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza pamoja na kupitishwa kwa Kanuni zinazokiongoza chombo hicho kama zilivyopendekezwa na klabu za Ligi Kuu na kupitishwa na Kamati ya Utendaji.

Mngongolwa aliendelea kusema kwa vile mapendekezo mawili kati ya matatu ya marekebisho ya Katiba yana uhusiano na Uchaguzi Mkuu wa TFF, kamati yake ikaona ipo haja ya marekebisho kufanyika kabla ya kutangazwa kwa Mkutano Mkuu wa TFF na kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF.


Aidha, kwa vile TFF haina uwezo wa kuitisha mikutano mikuu miwili – Mkutano Mkuu Maalum kwa ajili ya marekebisho ya Katiba ya TFF; na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi – katika kipindi kifupi kijacho, marekebisho ya Katiba yafanywe kwa njia ya Waraka (“Circular Resolution”).

Katika kipindi Novemba 15 mwaka huu  mwenyekiti wa kamati ya sheria na sekretarieti wataandaa waraka ambao utakabidhiwa kwa wajumbe wakamati ya utendaji ya TFF wanaowakilisha kanda na kuhakikisha kila mjumbe anapata fursa ya kutoa ridhaa yake na zoezi hili litadumu kwa siku 21 tu.

Baada ya hapo Kamati ya Utendaji itafanyika Jumamosi Desemba 15, mwaka huu kwa madhumuni ya kupokea taarifa ya zoezi hili na kufanya matayarisho ya Mkutano Mkuu.


Kutokana na Katiba ya TFF kuelekeza kuwa taarifa ya Mkutano Mkuu itolewe kwa wanachama wake angalau siku 60 (“notice period”) kabla ya Mkutano, Kamati ya utendaji inatarajia kuwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utafanyika Jumamosi na Jumapili ya tarehe 16 na 17 na Februari 2013.

Kamati ya Utendaji ya TFF inasisitiza kuwa utaratibu huu umeamuliwa kutokana na TFF kutokuwa na uwezo wa kifedha wa kutayarisha mikutano mikuu miwili katika kipindi kifupi kijacho. Kinyume chake ni kuchelewa zaidi kufanyika kwa Mkutano Mkuu, jambo ambalo hatuna budi kuliepuka.

Alimalizia kusema kuwa Kamati ya Utendaji inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na wadau wa mpira wa miguu kwa jumla ili kufanikisha zoezi hili na hatimaye kufanikisha Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa TFF.

No comments:

Post a Comment