Pages

Saturday, November 17, 2012

MWANAMBAYA MKURANGA WAANDAA BONANZA

UONGOZI wa Mwanambaya FC ya Mkuranga, Pwani umeandaa bonanza la mchezo wa soka litakaloanza Novemba 20 na kumalizika Novemba 24 mwaka huu.

Bonanza hili litafanyika kwenye uwanja wa Mwanambaya, Mkuranga na timu zilizoalikwa ni Afriroots Soccer Rangers na Salim FC za Dar es Salaam.

Timu ambazo zitafungua dimba siku ya jumanne ni Afriroots Soccer Rangers na Mwanambaya FC, jumatano  zitapambana Afriroots Soccer Rangers na Salim FC.

Novemba 24 uwanja wa Mwanambaya utawaka moto kwa Kombaini ya Mwanambaya kumenyana na Afriroots Soccer Rangers.

Akizungumza jijini Dar es salaam Mlezi wa Afriroots Soccer Academy Mwinyimad Tambaza alisema wamefurahi kualikwa kushiriki bonanza hilo kwani litawafanya kufahamiana na wachezaji wengine nje ya Dar es Salaam.

"Tunafurahi kualikwa kwenye bonanza hili na tutaenda kushiriki ili kuhamasisha michezo na kuongeza marafiki wa timu yetu", alisema Tambaza ambaye pia ni katibu wa chama cha kuendeleza Soka la vijana Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment