Pages

Friday, November 16, 2012

KUMBE CONGO BRAZAVILLE VIJEBA!

 
Timu ya soka ya vijana waliochini ya miaka 17 ya Tanzania bara Serengeti Boys jumapili itacheza dhidi ya timu ya vijana ya Congo Brazzaville uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Kocha Msaidizi wa Serengeti Boys Jamhuri Kihwelu 'Julio' amesema wataingia katika mchezo huo wakiwa na rufaa mkononi kutokana na kile alichokieleza kuwa wachezaji wengi wa Congo wanaonekana kama wana umri mkubwa.
 
Julio amesema amepata nafasi ya kuwaona wachezaji hao asubuhi ya leo wakati wakifanya mazoezi na ushahidi wa machoni unaonyesha wazi kuwa wachezaji hao wengi wao si chini ya umri wa miaka 17.
Julio amesema ana imani kuwa wachezaji waliopimwa vipimo vya umri na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF kwa siyo hao walikokuja nchini. 
Jana kocha Jacob Michelsen alisema ana wasiwasi wa kucheza na wachezaji vijeba ambao wengine walishiriki kombe la dunia mwaka jana na kutolewa katika hatua ya 16 bora na Uruguay, kimsingi amesema hilo analiacha kwa shirikisho la soka TFF.
 Lenzi ya Michezo  imejaribu kuperuzi mtandao wa shirikisho la soka duniani FIFA ambapo imebaini wachezaji wengine ni zaidi ya umri wa miaka 17. 

Katika kikosi kilichoshiriki kombe la dunia kwa vijana nchini Mexico kuna wachezaji 8 ambao wana umri zaidi ya miaka 17 ambao wamezaliwa si zaidi Oktoba, 1994 ambao kimsingi wamezidi umri wa miaka 17.
Wafuatao ni baadhi ya wachezaji waliozidi umri maana walishiriki kombe la dunia la vijana
1        Chill NGAKOSSO                   26/07/1994         GK          191
  2             Stevy SAMBA                     03/06/1994         DF           177
  3              Melvan LEKANDZA           02/04/1994         DF           186
4              Ange SITOU                        24/05/1994         MF         176
 5              Elvia IPAMY                        27/09/1994         FW         175
6            Gildas MPASSI                     10/01/1994           FW         175
 7             Gloire MAYANITH               13/10/1994         DF           181
8             Christ NKOUNKOU            27/07/1994         FW         180

Kikosi cha Congo Brazzaville kilicho shiriki kombe la dunia mwaka jana hiki hapa 

Nr.NameDate of BirthPositionHeight
1Chill NGAKOSSO26/07/1994GK191
2Cisse BASSOUMBA13/05/1996DF183
3Stevy SAMBA03/06/1994DF177
4Charvely MABIALA31/03/1996MF179
5Melvan LEKANDZA02/04/1994DF186
6Tierry KOUYIKOU17/01/1995MF177
7Ange SITOU24/05/1994MF176
8Hardy BINGUILA17/07/1996MF178
9Elvia IPAMY27/09/1994FW175
10Justalain KOUNKOU02/08/1996FW169
11Ramaric ETOU25/01/1995DF173
12Gildas MPASSI10/01/1994FW175
13Gloire MAYANITH13/10/1994DF181
14Christ NKOUNKOU27/07/1994FW180
17Bel EPAKO17/04/1995FW173
18Kader BIDIMBOU20/02/1996FW176
19Amour LOUSSOUKOU05/12/1996MF178
20Mavis TCHIBOTA07/05/1996FW177
21Pavelh NDZILA12/01/1995GK185

No comments:

Post a Comment