Pages

Thursday, November 1, 2012

MAVETERANI WA SIMBA USO KWA USO NA MAVETERANI WA MIRAMBO YA TABORA JUMAMOSI

MAVETERANI waliochezea timu ya Simba jumamosi watakuwa na mchezo wa kirafiki na maveterani wa timu ya Mirambo ya Tabora utakaochezwa uwanja wa shule ya msingi Makurumla uliopo Magomeni.

Akizungumza na LENZI YA MICHEZO Boniface Pawasa ambaye ni nahodha wa timu ya Simba alisema mchezo huo utaanza saa kumi jioni na kuwataka wachezaji wote kuhudhuria.

"Nawaomba wachezaji wote wa Simba na mashabiki wafike bila kukosa kupata burudani safi", alisema Pawasa.

Pia alisema kuwa mchezo huo ni maandalizi ya kujiweka sawa na bonanza la timu zilizowahi kucheza ligi daraja la kwanza kabla haijabadilika na kuwa
ligi kuu.

Bonanza la wachezaji wa timu zilizoshiriki ligi daraja la kwanza linatarajiwa kufanyika Novemba 11 mwaka huu kwenye viwanja vya Sigara.

Timu zinashiriki bonanza hili ni Simba, Yanga, Pan African, Nyota Nyekundu,  Pilsner, Sigara,  Reli Moro (kiboko cha vigogo), Tukuyu Stars, Coastal Union, Kariakoo ya Lindi na Mirambo ya Tabora. 

No comments:

Post a Comment