Pages

Thursday, November 1, 2012

DAMASI NDUMBARO AJIONDOA RUREFA

ALIYEKUWA anagombea nafasi ya Mwenyekiti kwenye uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Ruvuma, Damasi Ndumbaro amejiondoa.

Akizungumza na LENZI YA MICHEZO, Ndumbaro alisema amejiondoa kutokana na majukumu yake ya kazi kuongezeka kwa sasa hivyo itamwiwia vigumu kutekeleza yote kwa wakati mmoja.

"Nimeandika barua ya kujiondoa kutokana na majukumu yangu kuwa mengi kwani itaniwia vigumu kutekeleza yote kwa pamoja, pia naamini waliobaki wana uwezo wa kukisaidia chama"

Pia alisema pamoja na kuwa amejiondoa wagombea waliobaki wanauwezo wa kukiongoza chama vema na kuwatoa hofu wana Ruvuma.

Ndumbaro ambaye ana taaluma ya uanasheria na ni mwajiriwa wa shirika la Reli ya TAZARA amekuwa akitoa mchango wake kwenye soka kwa kupitia uwakala wa  wachezaji wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA)

No comments:

Post a Comment