Pages

Thursday, November 1, 2012

CANAVARO "UBINGWA WA VODACOM NI WETU"

Beki Nadir Haroub "Canavaro" akiwa na mshambuliaji  Simon Msuva 
"HAKUNA wa kutuzuia kuchukua ubingwa msimu huu", ndivyo alivyojigamba Nadir Haroub "Cannavaro" alipofanya mahojiano na LENZI YA MICHEZO  mara baada ya mchezo na Mgambo JKT kumalizika uwanja wa Taifa juzi.

Canavaro ambaye pia ni nahodha wa Yanga alisema kuwa walianza msimu vibaya lakini kwa sasa mafanikio yanaonekana wazi

"Unajua tulianza ligi kwa kususua lakini kwa sasa ubingwa unanukia kwetu", alisisitiza.

Beki huyu ambaye juzi alikuwa wa kwanza kuifungia timu yake bao la kwanza kwa kichwa dakika ya pili alicheza vema kwa kushirikiana na wachezaji wenzake na kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0.

Yanga inayonolewa na Ernest Brandts kwa sasa ina pointi 23 sawa na mahasimu wao Simba lakini wakitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufungwa na kufunga.

 Novemba 11 Yanga watakuwa wageni wa Coatal Union jijini Tanga kwenye uwanja wa Mkwakwani na Simba wataikaribisha Toto African ya Mwanza uwanja wa taifa.

Michezo hii miwili ndio itakayoamua nani anamaliza mzunguko wa kwanza akiwa kinara wa ligi kuu bara.



No comments:

Post a Comment