Pages
▼
Friday, November 16, 2012
CONGO BRAZAVILLE HAO KWENYE PICHA WAKIFANYA MAZOEZI KARUME
TIMU ya vijana waliochini ya 17 ya Congo Braza ville juzi waliwasili nchini tayari kwa mchezo wao na timu ya Taifa ya vijana walio chini ya miaka 17 "Serengeti boys" utakaochezwa jumapili hii uwanja wa taifa, jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo ambayo imekuja na wachezaji 18 na viongozi 12 wamefikia kwenye hotel ya Saphire
Tayari jana walifanya mazoezi kwenye uwanja wa Karume chini ya kocha wao Eddie Hudanski na msaidizi wake Basile Ekariki.
Timu hiyo imeundwa na wachezaji waliojengeka miili na warefu na wanaoneka wanaujua mpira kwa jinsi wanavyomiliki na kupiga mashuti.
Eddie Hudanski ambaye anazungumza kifaransa hakupenda kuzungumza na waandishi wa habari baada ya mazoezi kwa madai kuwa bado shirikisho la soka nchini halijampatia mkalimani.
No comments:
Post a Comment