Pages

Friday, November 16, 2012

KAMATI MAALUM YAZURU KAMBI YA SERENGETI



Kamati maalumu iliyoundwa na Rais wa shirikisho la soka hapa nchini Leodgar Tenga hii jana ilitembelea mazoezi ya timu ya taifa ya vijana waliochini ya miaka 17 yaliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Hiyo ilikuwa ni sehemu ya kuihamasisha timu ya vijana ya Serengeti Boys ili iweze kufanya vizuri katika mchezo wake wa jumapili dhidi ya timu ya Vijana ya Congo Brazzaville ambayo tayari imeshawasili nchini toka juzi usiku.

Akiongea na wachezaji hao Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Kassim Dewji amewataka wachezaji hao kuhakikisha wanazingatia maelekezo ya Kocha Jacob Michelsen akisaidiana na Jamhuri Kihwelu ili kuwa na nidhamu nzuri ya kimchezo na hatimaye kupata matokeo mazuri katika michezo yote miwili ya nyumbani na ugenini.

Dewji pia amewaambia wachezaji hao kuwa watanzania wanawategemea sana kuwapa ushindi katika mchezo huo na kwamba ana imani kubwa kuwa watajitokeza kwa wingi siku ya mchezo hivyo si vema wakaondoka uwanjani wakiinamisha vichwa chini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha hapa nchini Selemani Nyambui ambaye alipata nafasi ya kuongea na wachezaji hao amesema amefurahishwa sana na jinsi maandalizi ya mchezo huo yalivyo chukuliwa kwa uzito wa juu na hivyo ametaka wachezaji hao kuweka akili yote wanayofundishwa wa makocha wao.

Kambi ya timu ya taifa kuanzia hii juzi imehamia katika hoteli ya JB Belmont kwa lengo la kuongeza hamasa ya kambi ambapo jana wachezaji hao waliandaliwa chakula cha usiku katika mgahawa wa hoteli hiyo na wachezaji wakapata nafasi ya kubadilishana mawazo na wadau mbalimbali wa soka.

Mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana ya TFF Alhaji Ahmed Msafiri Mgoyi alisema maandalizi yanakwenda vizuri na kwamba leo waliwapokea waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Uganda na

No comments:

Post a Comment