TIMU ya Mbeya City jana ilimaliza mzunguko wa kwanza vema kwa kuifunga Majimaji bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Sokoine, Mbeya
Bao la Mbeya City lilifungwa na Deus Kaseke dakika ya 10 na lilidumu hadi dakika 90 ya mchezo.
Michezo mingine kwenye kundi A ilikuwa ni kati ya Mlale na Burkina Faso ambao walitoka sare ya 2-2 kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea na kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Mkamba walifungwa bao 1-0 na Kurugenzi ya Mafinga.
Kundi C ambalo limemaliza mzunguko wa kwanza lilikuwa na michezo minne kwenye viwanja vinne tofauti.
Kwenye uwanja CCM Kirumba, jijini Mwanza Pamba waliutumia vema uwanja wa nyumbani baada ya kuifunga Polisi Tabora mabao 2-1.
Uwanja wa Lake Tanganyika Kanembwa FC waliwachezesha kwata Polisi Mara kwa kuifunga bao 1-0 na Rhino ya Tabora ikaifunga Moran ya Kiteto nyumbani mabao 2-1.
Mkoani Shinyanga kwenye uwanja wa Kambarage wenyeji Mwadui waliifunga Polisi Dodoma mabao 4-0.
Kundi A na kundi c wamemaliza mzunguko wa kwanza juzi na kuacha kundi B likiendelea hadi Novemba 22, mwaka kutokana na michezo yao kusogezwa mbele kutokana na uhaba wa viwanja.
No comments:
Post a Comment