Pages

Monday, October 1, 2012

YANGA B YAINYUKA AFRICAN LYON B 3-1

TIMU B ya Yanga jana iliifunga timu B ya African Lyon bao 3-1 kwenye mchezo wa utangulizi uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga ambayo ilikuwa inashambulia sana lakini umakini wa washambuliaji ulikuwa mdogo walipata mabao yake kupitia kwa Abdallah Mguhi la pili alifunga Ussi Haji na karamu ya mabao iliitimishwa na Notkely Masasi.

Mchezo huo ambao ulikuwa ni utaratibu wa vilabu kuhakikisha wanatekeleza kanuni za ligi kuu ulikuwa kivutio kwa mashabiki wanaowahi uwanjani kwani walikuwa wanashangilia sana.

Salvatory Edward kocha wa Yanga alikisifu kikosi chake kwa mchezo mzuri waliocheza ila hakusita kusema kuna makosa ya kurekebisha.

"Timu imecheza vizuri na ushindi walistahili ila kuna makosa ambayo nitahitaji niyafanyie kazi ili yasijirudie tena", alisema Salvatory.

Upande wa African Lyon wachezaji walisema kuwa walijitahidi ila bahati haikuwa yao.

"Tumecheza vizuri lakini siku zote mpira una matokeo matatu na sisi tumefungwa hivyo tunachukulia kama changamoto kwetu" alisema mmoja wa wachezaji ambaye jina lake halikupatikana mara moja.

No comments:

Post a Comment