Pages
▼
Monday, October 1, 2012
HYPER FC BINGWA BEILA CUP
TIMU ya Hyper FC jana ilifunga Anta Shobo FC ya Gongolamboto kwa penalti 6-5 na kuchukua ubingwa wa mashindano ya Beila.
Fainali hizi za vijana wa U-14 zilichezwa uwanja wa Chanika uliopo nje ya manispaa ya Ilala kuanzia saa 10.00 jioni na zilihudhuriwa na mashabiki wengi.
Mchezo huo ulikuwa wa ushindani sana kwani dk 70 zilimalizika kwa suluhu ya 0-0 ndipo iliamuliwa zipigwe penalti. Kila timu ilipata penalti za awali ndipo ikaingia hatua ya kupiga penalti moja moja na Anta Shobo wakaondolewa.
Hyper FC bingwa wa Beila cup alipata zawadi ya Mbuzi mwenye thamani ya 60,000 na mshindi wa pili aliondoka na mpira mmoja
Timu ya Hyper Fc iliingia fainali baada ya kuifunga Italian Fc ya Chanika bao 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa uwanja huo wa Chanika na kuhudhuriwa na watazamaji wengi.
Nayo Anta Shobo wao waliifunga Kipawa Fc 4-1 na kufanikiwa kutinga fainali
Akizungumza na DIMBA Mratibu wa Mashindano Abdallah Kinyogoli alisema mashindano yalianza kutimua vumbi Septemba mosi mwaka huu na jumla timu 8 za vijana wa umri wa chini ya miaka 14 zilishiriki.
"Mashindano yalikuwa mazuri na nashukuru lengo la kuibua na kuendeleza vipaji limefanikiwa na nategemea kuanzisha mashindano mengine ili kuwapa fursa wachezaji chipukizi kucheza michezo mingi ili wapate uzoefu" alisema Abdallah.
No comments:
Post a Comment