Pages

Thursday, October 25, 2012

THOMAS ULIMWENGU APIGA HAT-TRICK


Ulimwengu akipongezwa na Tusilu



MSHAMBULIAJI chipukizi wa Kimataifa wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Thomas Ulimwengu jana aliifungia timu yake mabao 3 "hat-trick" dhidi ya 6 waliyoshinda dhidi ya Virunga katika mchezo wa Ligi Kuu ya nchini humo.

TP Mazembe iliandika bao la kwanza kupitia kwa Kanda Tisuli aliyepokea pasi safi toka kwa Thomas Ulimwengu dakika ya kwanza.

Katika dakika ya 20 Ulimwengu aliwanyanyua mashabiki wa timu hiyo, kufunga bao baada ya kuuwahi mpira ulikuwa unaelekea kuleta madhara langoni mwa wapinzani wao na mabeki wa Virunga kuzembea kuokoa.

Kama vile haitoshi dakika ya 29 Super Ulimwengu kama wanavyomwita wakongo alifunga bao lingine kabla ya kuitimisha lingine dakika ya 52.

Mshambuliaji Cheibane Traore alifunga bao la tano dakika ya 61 na karamu ya mabao ilihitimishwa na kiungo Mianga Ndonga

TP Mazembe wanakabiliwa na michezo miwili ya Lupopo na DCMP na kesho wanacheza na FC Saint Eloi Lupopo, mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Kibassa Maliba Lubumbashi na Oktoba 30, mwaka huu watacheza na DCMotema Pembe kwenye Uwanja wa Stade des Martrs Kinshasa.

No comments:

Post a Comment