Pages

Thursday, October 25, 2012

ASHANTI UNITED YAPIGA POLISI DAR MABOMU MAWILI

Ashanti United

























TIMU ya Ashanti United ya Ilala  imeifunga Polisi ya Dar es Salaam mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Karume jijini Dar es salaa.

Mchezo huo ulikuwa wa ushindani sana  hali iliyofanya timu zote kwenda mapumziko bila kufungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko lakini Ashanti ndio walionufaika baada ya kupata bao dakika ya 82 lililofungwa na nahodha wao Himidi Mohamed kwa njia ya penalti baada ya mchezaji wa Polisi kushika mpira eneo la penati.

Kama vile Ashanti ndio wamezinduka walijipatia bao la pili dk 89 kupitia kwa Shaban Juma kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Polisi.

Mpaka mwamuzi Hassan Mwinchumu anapuliza filimbi ya mwisho Ashanti 2 na Polisi 0.

Kocha wa Polisi Ngero Nyanjaba alilalamikia maamuzi ya mwamuzi kuwa aliwatoa wachezaji wake mchezo kwa faulo am,bazo anadai hazikuwa na umuhimu.

Naye Jamhuri Kiwelu "Julio" aliwapongeza wachezaji kwa kuanza ligi vema na kusema huo ni mwanzo mzuri na kuwataka wana Ilala kuisapoti timu yao ili iweze kufanya vizuri na hatimaye irudi ligi kuu.




























No comments:

Post a Comment