Pages

Wednesday, October 24, 2012

WAKATI YANGA IKITAKATA TAIFA, AZAM YABANWA NYUMBANI CHAMAZI


Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao alilifunga Didier Kavumbagu kwenye mchezo uliochezwa taifa dhidi ya Polisi Moro.





WAKATI Azam FC ikishikwa na Ruvu shooting kwa kufungana bao 1-1, timu ya Yanga SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa Polisi Morogoro mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huu Yanga inatimize pointi 17, baada ya kucheza mechi tisa na kuendelea kusimama katika nafasi ya tatu, nyuma ya Azam FC yenye pointi 18, baada ya sare ya 1-1 Ruvu shooting.
  
Bao la Ruvu shooting walipata bao lao kupitia kwa Seif Abdallah  na Azam walizawazisha bao lao kupitia Kipre Tcheche.

Mabao ya Yanga yalifungwa na washambuliaji Simon Msuva na Didier Kavumbangu kipindi cha kwanza.

Yanga walikosa penalti baada ya Haruna Niyonzima kupiga lakini shuti lake likagonga mwamba na kurudi uwanjani na kuokolewa na mabeki wa Polisi Morogoro.
   
Kipindi cha pili timu zote zilirudi na kushambuliana kwa zamu na madabiliko kadhaa lakini Yanga walitumia nafasi moja dakika ya 58, ambapo Hamisi Kiiza aliyeingia kuchukua nafasi ya Jerry Tegete alifunga bao la tatu.

Katika mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Coastal Union imeifunga 1-0 African Lyon kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mtibwa Sugar imelazimishwa sare ya 1-1 na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Kikosi cha Yanga leo; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Nahodha), Mbuyu Twite, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Jerry Tegete, Didier Kavumbangu na David Luhende.

Polisi; Manji Kulwa, Nahodha Bakari, John Bosco, Noel Msakwa, Salmin Kissi, Hamisi Mamiwa, Bantu Admin, Paschal Maige, Mokili Rambo (Nahodha), Malimi Busungu na Nicholas Kabipe.

No comments:

Post a Comment