Pages

Tuesday, October 23, 2012

OFISA HABARI WA TFF AULA CAF. FAINALI ZA WANAWAKE



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema  kuwa Ofisa Habari wake, Boniface Wambura ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) kuwa mmoja wa maofisa watakaoshughulikia masuala ya habari wakati wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika nchini Equatorial Guinea.
Uteuzi huo umefanywa na Rais wa CAF, Issa Hayatou kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji wa fainali hizo za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zilizopangwa kuanza Oktoba 28 mwaka huu na kumalizika Novemba 11 mwaka huu.
Wambura atakuwa mmoja wa maofisa watatu watakaoshughulikia habari kwenye fainali hizo. Wengine ni ofisa kutoka makao makuu ya CAF, Mahmoud Garga na Arlindo Macedo kutoka Angola.
Wambura atakuwa ni Mtanzania pekee kwenye Kamati ya Maandalizi ya fainali hizo, kitu ambacho TFF inajivunia kutoa mwakilishi kwenye moja ya mashindano makubwa ya mpira wa miguu Tanzania.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga ameelezea uteuzi  huyo kuwa ni matokeo ya kazi nzuri ambayo Wambura amekuwa akiifanya tangu ajiunge na Shirikisho Januari mwaka 2011.
“Taarifa zake mbalimbali zimeifanya Tanzania iwe inang’ara CAF na hata FIFA kwa kuwa kwa sasa wanajua kila kinachoendelea kwenye soka la Tanzania,” alisema Rais Tenga na kumtakia Wambura kila la kheri kwenye kazi hiyo atakayoifanya kwa takriban siku 14.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, akizungumza kwa niaba ya Sekretarieti, amemtakia Wambura kazi njema na kwamba awe kioo cha mabadiliko makubwa yanayoendelea kwenye soka la Tanzania.
Wambura alijiunga na TFF Januari, 2011 akiwa mmoja wa waajiriwa watatu wapya kwenye Shirikisho baada ya wsatendajiu wengine wawili kumaliza muda wao wa mikataba.
Wambura ni mwandishi wa habari mwandamizi ambaye ameshafanya kazi kwenye vyombo mbalimbali kuanzia kazi ya uandishi hadi Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jambo Leo ambalo alikuwa akifanya kazi kabla ya kujiunga na TFF
ORODHA YA WAHUSIKA WOTE HII HAPA

CONFEDERATION AFRICAINE DE FOOTBALL
3 Abdel Khalek Tharwat Street, El Hay El Motamayez, P.O. Box 23
6th October City, Egypt.
Tel.: 202 3837 1000 / Fax : 202 3837 0006
CAF DELEGATION FOR THE 8th AFRICAN WOMEN CHAMPIONSHIP
EQUATORIAL GUINEA, MALABO & BATA - 28 Oct. – 11 Nov. 2012
CAF President: Issa Hayatou (Cameroon)
CAF General Secretary Hicham El Amrani (Morocco) - partly
Organising Committee for Women
Molefi Oliphant (South Africa) President
Nastasia Tchislas (South Africa) Vice-President
Izzetta Wesley (Liberia) Member
Palmira Francisco (Mozambique) Member
Ibrahima Barry (Guinea) Member
Lydia Nsekera (Burundi) Member
John Muinjo (Namibia) Member
Souadatou Djallo-Kalkaba (Cameroon) Member
Nathalie Basque (Côte d’Ivoire) Member
Mariyatta Abdou Chacour (Comoros) Member
Hilda Addah (Ghana) Member
Beatrice Nsolo (Gabon) Member
Disciplinary Board
M. Augustin Emmanuel Senghor (Senegal) Chairman
George William Wah (Liberia) Member
Board of Appeal
Prosper Abega (Cameroon) Chairman
Referees’ Committee
Tarek Bouchamaoui (Tunisia) Chairman
Sinko Zeli (Côte d'Ivoire) Member
Kalombo Bester (CAF) CAF Refereeing Manager
Medical Committee
Adoum Djibrine (Tchad) Chairman
Dr. Zakia Bartagi (Tunisia) Member
Dr. Moolla (South Africa) Member
CONFEDERATION AFRICAINE DE FOOTBALL
3 Abdel Khalek Tharwat Street, El Hay El Motamayez, P.O. Box 23
6th October City, Egypt.
Tel.: 202 3837 1000 / Fax : 202 3837 0006
Technical Study Group
Fran Hilton Smith (South Africa) Member
Jacquelline Shipanga (Namibia) Member
General Coordinators
Sue Destombes (South Africa) Group A
Djibril Traore (Mali) Group B
Assistant General Coordinators
Alex Asante (Ghana) Group A
Yaouba Hamoa (Cameroon) Group B
Media Officers
Mahmoud Garga (CAF)
Boniface Wambura (Tanzania)
Arlindo Macedo (Angola)
Presidential Office
Ibrahim Kouramou (Cameroon) Attaché
Baba Mohammadou (Cameroon) Attaché
Richard Ngue (Cameroon) Attaché
Seidou Mbombo Njoya (Cameroon Protocol
CAF Secretariat
Essam Ahmed Deputy Secretary General
Heba Abdallah Event Director and Senior Manager of
Women competitions
Khaled Nassar Assistant to the Event Director
Amr Shaheen Marketing Director
Inas Fahmy Travel Manager
Mohamed Sherei Finance Deputy Director
Fayez Nahal Accounting Manager
Amina Kassem Head of Disciplinary sector & event secretary
Sherif Ahmed Doping matters and Transport

No comments:

Post a Comment