Pages

Tuesday, October 23, 2012

BONANZA LA WACHEZAJI WA ZAMANI LAJA

KAMATI inayoratibu bonanza linaloshirikisha wachezaji waliochezea timu za ligi daraja ligi kuu (zamani daraja la kwanza) kuwa bonanza litafanyika Novemba 4 mwaka huu kwenye viwanja vya Bandari Kurasini, Temeke.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katibu wa kamati hiyo Wilfred Kidau amesema tarehe ya bonanza ni Novemba 4 mwaka huu kwenye viwanja vya bandari Temeke na jumla ya timu 12 zitashiriki.

Pia amesema kila timu iwakumbushe wachezaji wafanye mazoezi ili kujiweka sawa kuhakikisha siku ya bonanza wanawapa burudani na ladha halisi ya uchezaji wa zamani mashabiki.

"Bonanza litakuwa linashirikisha wachezaji wa zamani walicheza ligi daraja la kwanza miaka 1996 kurudi nyuma na litaanza asubuhi hadi jioni.

Kidau ambaye atachezea Mirambo ya Tabora anawataka mashabiki na wapenda soka wote wafike viwanja vya Bandari kurasini ili wapate burudani safi na kuwapa sapoti wachezaji wanaowapenda.

Timu zinashoriki bonanza hili ni Simba, Yanga, Pan African, Nyota Nyekundu,  Pilsner, Sigara,  Reli Moro (kiboko cha vigogo), Tukuyu Stars, Coastal Union, Kariakoo ya Lindi na Mirambo ya Tabora. 

No comments:

Post a Comment