Pages

Sunday, October 28, 2012

NNAMPUNDE ABWAGWA NA KATIBU WAKE FRANCIS NDULANE

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha soka Lindi (LIREFA) na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) Alhaj Shaib Nnampunde ameangushwa vibaya kwenye uchaguzi wa chama hicho na aliyekuwa Katibu wake Francis Ndulane.

Uchaguzi huo ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa chama cha waalimu (CWT) Ruangwa, Nnampunde ambaye alikuwa anatetea nafasi yake ya Mwenyekiti aliambulia kura mbili dhidi ya kura 14 alizopata Francis Ndulane na kufatiwa na Tumaini Kagina aliyepata kura kumi.

Francis Ndulane ambaye amekuwa Katibu wa LIREFA kwa miaka minne alitangazwa rasmi na Katibu wa kamati ya uchaguzi ndugu Mohamed Kambwilina kushuhudiwa na Francis Lyato ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya TFF.

Nafasi ya Katibu iliwenda kwa Louis Taisamo aliyepata kura 14 na kufuatiwa na mpinzani wake aliyepata kura 11.

Mgombea pekee wa nafasi Mwekahazina Vicent Fikiri alipata kura 14 za ndiyo na 12 za hapana na Mkutano mkuu wa TFF ilichukuliwa na mwana mama Zafarani Damoda aliyepata kura 18 na kumwangusha Ally Kamtende aliyepata kura saba.

Nafasi ya Mwakilishi wa Vilabu ilichukuliwa na Dastan Mkundi kwa kura 15 dhidi ya kura kumi za Steven Nyoni.

Nafasi za Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya utendaji hazikupata wagombea kutokana na kukosa sifa huku nafasi ya Katibu Msaidizi nayo ikikosa mtu baada ya mgombea pekee Akida  Said kupata kura 9 za ndiyo na kura 17 za hapana.

No comments:

Post a Comment