Pages

Sunday, October 28, 2012

BFT YAPOKEA MSAADA TOKA KWA IDD AZAN

Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) jana lilipatiwa msaada wa vifaa mbalimbali vya ngumi na Mh. Iddi Azan (MB) Kinondoni.

Hafla hiyo ya kukabidhi Vifaa hivyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Msasani klabu na thamani yake ni Tshs 2,000,000/=.

Akiongea wakati wa kupokea vifaa hivyo Katibu Mkuu wa BFT Makore Mashaga kwa niaba ya kamati ya maandalizi, alimshukuru sana Mh. Iddi Azan kwa jinsi alivyoguswa na kuona umuhimu wa kusaidia timu ya taifa ya ngumi


Pia alisema timu inahitaji mazoezi na mashindano ya uhakika ili mabondia hao wapate uzoefu wa kimataifa kabla ya kushiriki mashindano makubwa ya kimataifa kama ya Jumuiya ya Madola, Afrika,ubingwa wa Dunia na Olimpiki.

Pia alisema msaada huo umekuja wakati mwafaka kwa kuwa baadhi ya vifaa hivyo vitatumika katika mashindano ya kimataifa ya kirafiki kati ya timu ya taifa ya Tanzania na Zambia yatakayofanyika Novemba 3 mwaka huu katika ukumbi wa DDC kariakoo kuanzia saa 9.00 Alasiri.

Nae Mh.Iddi Azan akiongea wakati wa Makabidhiano hayo alisema yeye ameguswa na kuona umuhimu wa kusaidia timu ya taifa ya ngumi kwa kuwa ni moja ya mchezo ambao umekuwa ikiwakilisha taifa la Tanzania katika mashindano mengi ya kimataifa.

Pia ni  mchezo ambao imeshaitangaza Tanzania kimataifa kwa kuleta medali mbalimbali katika mashindano ya ubingwa wa dunia ,mashindano ya jumuiya ya madola,mashindano ya Afrika,mashindano ya afrika mashariki kati na & kusini na mengine mengi.


Vifaa vilivyokabidhiwa ni Gloves pair 10, Heard guards 15, mouth guards 20 na clip bandage 15.

No comments:

Post a Comment