Pages

Wednesday, October 3, 2012

MUDA WA PRESHA ZA MASHABIKI KARIBIA UNAWADIA

MIEZI, wiki, siku, saa na sasa dakika zilizokuwa zinasubiriwa kwa hamu hatimaye umewadia.
Ni mpambano ambao kwa vyoyote vile mtoto hatumwi sokoni kwani upande mmoja unasaka kuendeleza kulinda heshima ya bao 5-0 na upande wa pili unatafuta kuondoa au kupunguza idadi hizo za mabao.

Mimi siyo mtabiri wa nani atashinda ila dakika 90 ndizo zitakazoamua nani ni nani.
Nijuavyo mpambano wa leo kama itatokea upande mmoja ukafungwa sishangai kuona watu wakiwa wamezimia.

Simba wanaingia uwanjani wakiwa na pointi 12 baada ya kushinda michezo yao minne na Yanga wao wana pointi 7 wakiwa wamecheza michezo minne kushinda miwili, kutoka sare mmoja na kufungwa mmoja na ipo nafasi ya nne.

Kikosi cha Yanga kipo imara na hakina majeruhi wakati Simba wao wanamkosa mshambuliaji wao wa kimataofa toka Uganda Emanuel Okwi na Amir Maftah ambao wanatumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Makocha wa timu hizi wote wanasema wanashinda mchezo huu unaotarajiwa kuanza takribani saa mbili zijazo na kila mmoja akijisifu anakiamini kikosi chake.

Mimi na wewe twende tukashuhudie nani ni nani kwenye uwanja mkuu wa Taifa majira ya saa moja nyasi zitakapoanza kuwaka moto.

No comments:

Post a Comment