Pages

Monday, October 1, 2012

BOBAN AREJEA SIMBA KUIVAA YANGA



Haruna Moshi "Boban"


KIUNGO Mshambuliaji wa Simba Haruna Moshi 'Boban' ameshusha presha ya
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Milovan Cirkovic baada ya juzi usiku kuanza
mazoezi na wenzake kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu
Tanzania Bara dhidi ya Yanga, utakaochezwa kesho Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.

Babon ambaye aliwasili mjini hapa juzi mchana kwa Ndege alikuwa
anasubuliwa na malaria  hivyo kumfanya ashindwe kucheza katika
mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons uliopigwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jiini Dar es Salaam.

Simba ambayo imeweka kambi Zanzibar, ikijiandaa na mchezo huo itakuwa kwenye nafasi nzuri na utulivu baada ya kurejea kwa Babon katika kikosi hicho ambacho kinatawakosa nyota wake wawili tegemeo wanaotumikia adhabu ya kadi nyekundu Emmamuel Okwi na Amir Maftah.

Hata hivyo, mazoezi ya timu hiyo juzi yaliingia dosari baada ya umeme
kukatika ghafla katika Uwanja wa Amani na kushindwa kuanza kwa wakati
uliopangwa.

Wachezaji hao ambao walikuwa chini ya Kocha Msaidizi Richard Amatre
 raia wa Uganda, waliingia uwanjani saa moja lakini umeme ulikatika wakiwa wameanza
mazoezi ya kupasha misuli.

Kutokana na tukio hilo, wachezaji hao walitakiwa kusubiri kwa muda wa
takribani  saa moja kabla ya umeme kurudi na baadaye walicheza mchezo
wa kirafiki dhidi Zanzibar All Stars.

Mchezo huo ulianza saa 2.50  usiku na timu hizo zilitoka suluhu ambapo
baadhi ya wachezaji wa Simba akiwemo Juma Kaseja, Felix Sunzu, Edward
Christopher na Shomari Kapombe hawakucheza.

No comments:

Post a Comment