Pages

Monday, October 1, 2012

MLOKOLE KUCHEZESHA SIMBA NA YANGA


MWAMUZI Mathew Akrama kutoka jijini Mwanza ameteuliwa kuchezesha pambano la watani wa jadi la Simba na Yanga litakalofanyika keshokutwa katika Uwanja wa Taifa  huku taarifa zikieleza kwamba ni muumini wa dhehebu la kilokole.


Taarifa kutoka kwa rafiki wa karibu wa mwamuzi huyo zinasema kwamba Akrama ni muumini mzuri wa kanisa la kilokole huku akitumia muda wake wa ziada anaupata nje ya uamuzi katika uimbaji.

“Akrama ni muumini mzuri wa kanisa la kilokole la EAGT na ni mtu wa kazi hawezi kupokea rushwa hata kidogo kutokana na msimamo wake kidini.

“Kwa msimamo wake ni dhahiri kwamba maamuzi yake yanaweza kuwa bora na tofauti na yale tunayoyaona katika baadhi ya viwanja kwa hiyo katika hili hakuna tatizo,” alisema rafiki huyo ambaye kitaaluma ni mwamuzi pia.

Jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema kuwa Akrama atakuwa mwamuzi wa kati wa pambano hilo ambalo linaendelea kuvuta hisia za mashabiki wa soka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

“ Akrama atasaidiwa na Samuel Mpenzu kutoka Arusha na Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam huku mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga kutoka Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment