Pages

Tuesday, October 23, 2012

JULIO AWAPASHA VIONGOZI WA TANZANIA

KOCHA msaidizi wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) Jamhuri Kiwelu "Julio" amewataka viongozi kuisaidia timu hiyo ili iweze kufuzu fainali za vijana zinazotarjiwa kufanyika Machi mwakani nchini Morocco.

Julio aliyasema hayo juzi jioni wakati wakiwa mazoezini kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam ikiwa ndio wameingia kambini baada ya kambi kuvunjwa kwa wiki mbili baada ya kufuzu kwa awamu a tatu na ya mwisho.

"Viongozi wetu wasiwe watu bwa kuja kukabidhi bendera tu timu inaposafiri maana bendera mtu yeyote anaweza kukabidhi, ila wanatakiwa kutembelea kambi kujua timu inaendeleaje na kuipa misaada maana haina mfadhili na TFF hawana fedha ya kuihudumia", alisema Julio kocha mwenye maneno mengi.

Pia alisema timu ina nafasi nzuri ya kusonga mbele hivyo wakati huu ndio muafaka wa kuisadia na siyo wangoje ikiwa imefuzu ndio wanaanza kuisaidia.

Serengeti Boys ambayo iko chini ya Kocha Jakob Michelsen itacheza mechi hiyo ya raundi ya tatu na mshindi kati ya Congo Brazzaville na Zimbabwe ambapo tayari Congo Brazzaville imefanikiwa kupata ushindi wa ugenini wa mabao 2-1.

Mechi ya marudiano itachezwa jijini Brazzaville kati ya Oktoba 26-28 mwaka huu.

Katika mechi hiyo ya raundi ya tatu, Serengeti Boys itaanzia nyumbani katika mchezo utakaofanyika Novemba 17 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, wakati mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liko katika mikakati ya kuhakikisha Serengeti Boys inapata mechi mbili za kirafiki za kimataifa kabla ya kumvaa mshindi kati ya Congo Brazzaville na Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment