Pages

Sunday, September 30, 2012

FRANCIS CHEKA AMTWANGA KARAMA NYILAWILA KWA KO

BONDIA Francis Cheka jana usiku alimpiga kwa KO bondia Karama Nyilawila kwenye pambano la raundi 12 la UBO

Cheka alimpiga Nyilawila kwa KO raundi ya sita alipomtwanga ngumi iliyompeleka chini na kumfanya refa kumwehesabia lakini aliponyanyuka aliamua kuvua gloves kuahashiria amekubali matokeo.

Cheka ambaye aliingia ulingoni bila mbwembwe alimwacha Nyilawila ajifurahishe kwa kurusha makonde ambayo alikuwa anayakwepa hivyo kumfanya pumzi kumwishia mapema.

Ilipotimu raundi ya tano Cheka alianza kurusha ngumi nzito nzito na kufanya ukumbi kulipuka kwa kelele za kusema " Cheka ua huyo unampotezea muda, maliza"

Karama Nyilawila akiwa amekaa baada ya kupokea konde takatifu kutoka kwa Francis Cheka


Francis Cheka akipangua ngumi ya Karama Nyilawila

Bondia Karama Nyilawila akiwa amemkumbatia Francis Cheka
Karama ambaye aliingia ukumbi kwa mbwembwe huku akisindikizwa na mabausa alijikuta akiondoka mnyonge baada ya kuonjeshwa makonde ya haja.

No comments:

Post a Comment