Pages

Sunday, September 30, 2012

NIZAR NOMA ATUPIA MBILI YANGA IKIIKABILI AFRICAN LYON

TIMU ya Yanga leo imeifunga African Lyon bao 3-1 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania, mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.
Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa nahodha wao Nadir Haroub "Canavaro" baada ya kuwaahadaa mabeki wa African Lyon.
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Yanga walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0

Kipindi cha pili timu zote ziliingia uwanjani zikiwa na matumaini mapya kwani kila timu ilikuwa inashambulia kupata bao.
Benedicto Mwamlangala alifanya kazi nzuri sana na kuifungia African Lyon bao la kusawazisha lakini kabla hawajajipanga kuleta mashambulizi Nizar Khalfan alileta kilio langoni mwa Lyon baada ya kufunga bao la pili.
Kama hiyo haitoshi Yanga waliendeleza mashambulizi hadi kwenye eneo la penalti watoto wa mjini wanaita sita na kufunga bao nzuri sana na kushangilia kwa staili ya kusujudu.
African Lyon watajilaumu kwa kupoteza mchezo huu kwani walicheza vizuri ila kutojaribu wakiwa mbali ndicho kilichowagharimu.
Hamis Kiiza akimtoka beki wa Lyon Sunday Bakari kwenye mchezo wa VPL uliochezwa uwanja wa taifa, Yanga ilishinda 3-1




Staili ya Nizar akishangilia bao la pili alilofunga yeye lakini la tatu kwa mchezo huo


No comments:

Post a Comment