YANGA imepata ushindi wa kwanza wa michuano
ya Kombe la Mpumalanga baada ya kuafunga wenyeji wao Tx Galaxy kwa bao 1-0 katika
Uwanja wa Mbombela, Afrika Kusini leo
Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na
Prince Dube dakika ya 55 lakini pia Galaxy
walipata penalti dakika ya 73, wakakosa.
Kwa matokeo
hayo Yanga ina pointi tatu sawa na Augsburg ya Ujerumani ambao walishinda 2-1
dhidi ya Yanga.
Usajili mpya wa Yanga unaonekana kuwa na
tija kwani mabao katika michezo yaote yamefungwa na Jean Baleke ambaye
amesajiliwa kwa mkopo kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC) na Dube kutoka Azam FC.
Yanga wanatumia michuano hiyo kama sehemu
ya matayarisho ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa.
Yanga watakamilisha ziara yao nchini humo
kwa kuikabili Kaizer Chiefs kwenye michuano ya Kombe la Toyota Julai 28 mwaka
huu na wanatarajia kurejea nchini Julai 30 kwa maandalizi ya Kilele cha Wiki ya
Mwanachi, Agosti 3, mwaka huu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment