Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, April 22, 2018

MTIBWA YAFUNGUKA KUSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA


Na Rahel Pallangyo
HATIMAYE uongozi wa Mtibwa Sugar umefunguka na kudai itashiriki michuano ya Afrika mwakani endapo itafuzu, kwa sababu adhabu yao walishaimalizika
Awali kulikuwepo na minong’ono kuwa Mtibwa Sugar haiwezi kushiriki mashindano ya Afrika kwa sababu walifungiwa na Shirikisho la Soka Barani hivyo haitashiriki michuano ya Afrika hata ikifuzu. 
Katibu Msaidizi wa timu hiyo, Abubakar Swabur alisema hizo propaganda wamezisikia na kudai ni za uoongo kwani walifungiwa mwaka 2004 na kwa maana hiyo walimaliza adhabu 2007 kwani walifungiwa miaka mitatu.
 “Kumekuwepo na propaganda kuwa Mtibwa Sugar haitashiriki mashindano ya kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la soka Afrika (CAF), kitu ambacho ni uongo za inabidi upuuzwe kwani hauna ukweli wowote. Ni kweli Mtibwa Sugar ilifungiwa miaka mitatu na kupigwa faini ya fedha mwaka 2004,” alisema Abubakar 
Abubalar alisema inasemekana Mtibwa Sugar haiwezi kushiriki kutokana kwa sababu adhabu unaanza kuitumikia iwapo klabu itafuzu michuano hiyo na Mtibwa Sugar haijawahi kufuzu michuano hiyo tangu ifungiwe na kudai siyo kweli yanalenga kuwatoa katika njia ya ubingwa kwani kauli mbiu yao inasema "Heshima ya 1999-2000  irejee".
 Pia alisema timu yeyote ikifungiwa kutokana na michuano inayoratibiwa na CAF inaanza kutumikia adhabu hiyo baada ya kupokea taarifa hiyo na haisubiri hadi ikifuzu kwa maana nyingine adhabu hiyo siyo lazima ufuzu ndiyo uitumikie.
“Kwa wanasheria kuna kitu kinaitwa rejea katika kuamua kesi zenye mazingira yanayofanana na suala la Mtibwa Sugar naomba nije na na rejea ya kesi zinazofanana na hukumu iliyotolewa na CAF kwa Mtibwa Sugar, Highlanders ya Zimbabwe ilifungiwa na CAF miaka mitatu  kwa kushindwa kusafiri kucheza na Nchanga Rangers ya Zambia na adhabu hiyo walianza kuitumikia mwaka 2012 na baada ya miaka miwili Highlanders kupitia ZIFA (Shirikisho la Soka Zimbabwe) wakaomba kupewa msamaha, CAF waliwajibu adhabu inaisha mwaka 2015, wavumilie,” alisema Abubakari.
Pia Mwaka 2012, Abeid Pele na timu yake ya Nania FC ya Ghana walifungiwa miaka mitatu na kupigwa faini ya dola za Kimarekanio 1,500 na CAF walionyesha adhabu hiyo inaisha mwaka 2016, hivyo CAF walikuwa wanajua hawa jamaa watafuzu mara zote, au? 
Keizer Chiefs ya Afrika Kusini nayo mwaka 2004 ilifungiwa miaka mitatu na kupigwa faini ya dola 1,500 kwa kushindwa kusafiri kwenda kucheza mchezo wa marudiano na Esperance ya Tunisia baada ya kufungwa mchezo wa kwanza nyumbani. Na wakati adhabu yao inaisha walikuwa nafasi ya 11 katika msimamo wa Ligi Kuu Afrika Kusini, ambayo haiwapi fursa ya kushiriki michuano hiyo ya kimataifa na adhabu yao ilimalizika wakiwa hawapo kwenye nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.
Abubakar alisema Mtibwa Sugar wanajipanga kwa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) unaotarajiwa kuchezwa Juni 2, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha kwani wakishinda watapata tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.