Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 14, 2018

YANGA YAZIDI KUNOGA, YAIADHIBU MAJIMAJI 4-1 UWANJA WA TAIFA



MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Yanga, leo wamezidi kujiimarisha katika kutetea ubingwa huo baada ya kushuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Majimaji.
Katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Yanga ilitawala karibu kila eneo katika vipindi vyote.
Yanga ilipata bao la kuongoza katika dakika ya 20 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na Pappy Tshishimbi.
Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi Nassoro Mwinchui wa Pwani baada ya Mpoki Mwakinyuke wa Majimaji kushika mpira kwa mkono akimzuia Obrey Shirwa kufunga wakati kipa wa Majimaji Salehe Malande akiwa ameanguka.
Kutokana na kosa hilo, mwamuzi alimuonesha Mwakinyuke kadi nyekundu.
Dakika tisa baadaye, Chirwa aliiandikia Yanga bao la pili akiunganisha krosi ya Gadiel Michael.
Dakika mbili kabla ya kwenda mapumziko Emmanuel Martin alifunga bao la tatu kwa shuti kali nje ya 18 lililotinga moja kwa moja wavuni.
Kipindi cha pili kilianza kwa Majimaji kutaka kuresha bao na jitihada zao zilianza kuzaa matunda baada ya kupata penalti katika dakika ya 56 na Marcel Bonavanture kuukwamisha mpira wavuni.
Mwamuzi Mwanchui alitoa penalti hiyo baada ya Saidi Makapu wa Yanga kushika mpira eneo la hatari.
Tshishimbi aliwainua tena mashabiki wa Yanga katika dakika ya 85 alipoandika bao la nne kwa shuti kali karibu na 18 na kujaa wavuni.
Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 37 nyuma ya kinara Simba iliyo kileleni kwa Pointi 41.

Aidha, matokeo hayo yamezidisha presha kwa Simba iliyo ugenini Shinyanga leo kucheza dhidi ya Mwadui ambapo salama yake ni ushindi ili iendelee kujiimarisha.

No comments:

Post a Comment