KAMATI ya
Utendaji ya klabu ya Simba imeunda Kamati ya watu watano kusimamia mchakato wa
zabuni kuwapata wawekezaji ambao ni wanachama wa klabu hiyo watakaonunua
asilimia 50 ya hisa zao.
Hatua hiyo
imetangazwa jana Dar es Salaam baada ya kamati kukutana kujadili mchakato wa
kubadilisha muundo wa uendeshaji kufuatia wanachama 1,200 kupitisha kwenye
mkutano wa wanachama uliofanyika Agosti 20, 2017.
Katibu Mkuu
wa Simba, Dk Arnold Kashembe alisema kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti, Jaji
mstaafu Thomas Mihayo ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini (TTB).
Wajumbe ni
Wakili Damas Ndumbaro, Azzan Zungu ambaye ni Mbunge wa Ilala, Abdulrazaq Badru
ambaye ni Mkurugenzi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini na Dk Yusuf
Majid, mtaalamu wa masuala ya ununuzi nchini.
Mkuu wa
Idara ya Habari Simba, Haji Manara alifafanua kuwa katika asilimia 100 za hisa,
50 zinatakiwa ziuzwe kwa mwanachama wa Simba katika mfumo wa tenda na 50
zilizobaki hisa 10 zitakuwa za wanachama na 40 zitakuwa mtaji.
"Kamati
haitaingiliwa na mtu kwani itafanya kazi kwa mujibu wa sheria za manunuzi ya
umma na za nchi hii na mshindi atatangazwa na jina lake kupelekwa kwa
wanachama," alisema.
Manara
amewahimiza wanachama wa Simba wenye uwezo wa kununua hisa wajitokeze na
kufanya uwekezaji huo kwa manufaa ya klabu.
Katika hatua
nyingine, Manara ameiomba Serikali kushirikiana nao kuwakamata watu wanaouza
jezi bandia mtaani na mechi za soka
uwanja wa Taifa ili wachukuliwe hatua kali.
"Kama
Serikali ilishirikiana na wasanii kudhibiti CD bandia, inaweza kushirikiana na
sisi kudhibiti jezi bandia kwa sababu wako wauzaji wengi wanatunyima
mapato," alisema.

No comments:
Post a Comment