Kwa mujibu
wa ratiba ya awali ambayo uongozi mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
iliunda kikosi kazi kwa ajili ya kuipitia kwa sababu ya kuwa na mapungufu
mengi, mchezo huo ulikuwa huchezwa Oktoba 14 na Simba ndio alikuwa mwenyeji.
Raundi ya
pili zitakutana raundi ya 23 ambayo inataanza Machi 14 lakini haujapangiwa
tarehe wakati awali zilikuwa zikutane raundi Machi 3, 2018
Pazia la
ligi linatarajiwa kufungwa Mei 26, ambapo Simba itamaliza ugenini kwa kucheza
na Majimaji na Yanga itamaza nyumbani kwa kucheza na Azam FC
Ofisa habari
wa TFF, Alfred Lucas alisema mchezo wa Simba na Yanga umesogezwa mbele kwa 14 katika
raundi ya nane na dirisha dogo
linatarajiwa kufunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15.
“Ratiba
imebadilika kwa kiasi kikubwa kwani kwa mujibu wa ratiba ya awali ligi ilikuwa
imalizike Mei 5, 2018 lakini sasa itamalizika Mei 28, 2018 siku 21 zaidi,”
alisema Lucas.
Pia Lucas
alisema raundi ya pili itaanza Januari 19, 2018 badala ya Disemba 30, 2017 kama
ratiba ya awali ilivyoonesha.
Baada
ya michezo ya Agosti 26 na 27, Ligi Kuu ya sasa itaendelea Septemba 9 na 10 kwa
michezo nane kuchezwa katika viwanja tofauti.
No comments:
Post a Comment