SERIKALI
imesema ipo tayari kwa ajili ya kuwa wenyeji wa mashindano ya Vijana ya Afrika
waliochini ya Umri wa miaka 17 (AFCON U-17) yanayotarajiwa kufanyika 2019 hivyo
Watanzania wasiwe na wasiwasi.
Hayo yalisemwa
leo na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe
wakati akipokea taarifa ya maandalizi kutoka Shikirisho la Soka Tanzania (TFF)
hafla iliyofanyika Dar es Salaam.
‘Sisi
wenyewe serikali ndio tuliandika barua Shirikisho la Soka barani Afrika
(CAF) na kusema tunaomba kuandaa fainali
za Vijana za Afrika kama nchi zingine zinavyofanya na mwaka 2015
tulikubaliwa,” alisema Dk. Mwakyembe.
Alisema
anashukuru kuona maandalizi yalianza mapema na sasa Tanzania ina timu nzuri
ambayo inatarajiwa kuleta ushindani na kusema usalama wa kutosha upo, hoteli na
barabara zitakazopita magari wakati wa kwenda uwanjani na mazoezini zinafanyiwa
kazi.
“Jana (juzi) nilitembelea Uwanja wa Taifa
ambao upo kwenye marekebisho na sasa unaendelea vizuri na nataka ukikamilika utiwe
kufuli wakati tunaendelea na kuandaa viwanja vingine,” alisema Dk. Mwakyembe
Pia alisema
sehemu ya vyumba vya kubadilishia nguo imekamilika na kusema kutakuwepo na hoteli
ndani ya uwanja wa Taifa ambayo itakuwa inatoa huduma kipindi chote na kusema
ataendelea kushirikiana na sekta binafsi kuona fainali hizo zinafanikiwa kwa
kiasi kikubwa.
Dk.
Mwakyembe alitumia fursa hiyo kumpongeza mjumbe wa heshima wa CAF, Leodgar
Tenga kwa namna ambavyo amekuwa akiiwakilisha vema Tanzania katika soka kwani
amekuwa akitetea nchi za
Awali
akizungumza, Mjumbe wa heshima wa Caf, Leodgar Tenga alisema kwa asilimia kubwa
Tanzania imefanya maandalizi makubwa na ana uhakika sasa mashindano yatafanyika
‘’Sisi wengine tunaona fahari kuandaa
mashindano haya kwani nchi haijawahi kufanya hivyo, na CAF wana matumaini
makubwa maana tuna uwanja mzuri, tuna mashabiki na sifa ya amani nayo
inatupaisha,” alisema Tenga.
Tenga
alisema Caf ina uhakika mashabiki watakuja na kurejea chini mwao wakiwa salama kwa sababu Tanzania
ni nchi ya amani nanajisikia fahari kuwa sehemu yake.
Aidha Tenga
alisema CAF imepandisha viwango kwa ajili ya kupandisha soka la Afrika hivyo kufanikiwa
kuandaa fainali za vijana itasaidia kuitangaza nchi na bara la Afrika.
Hafla
hiyo pia ilihudhuriwa na Mkurungenzi wa Maendeleo ya Michezo Dk. Yusuph Singo, Rais
wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia, , Kaimu Katibu Mkuu wa TFF,
Kidao Wilfred, Mkurengezi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi, Henry Tandau,
Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kasongo na wajumbe wa kamati ya ufundi
No comments:
Post a Comment