KOCHA wa
Simba, Joseph Omog katika kutatua tatizo la umalizia wa safu ya ushambuliaji
ameibadilishia mfumo Mwadui FC na sasa inaonekana atatumia zaidi mabeki wa
pembeni kuanzisha mashambulizi na
mawinga wakiingia kati kujumuika na washambuliaji kumalizia.
Hayo
yalionekana katika mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jana
na leo kocha Omog alitumia zaidi ya dakika 30 kuwaelekeza mabeki Ally Shomari na
Mohammed Hussein kuanzisha kwa kasi mashambulizi kutoka pembeni na kupiga krosi
kwa washambuliaji John Bocco na Emmanuel Okwi huku mawinga Shiza Kichuya na
Mohammed Ibrahim nao wakiingia ndani.
Katika
mazoezi hayo Omog alionyesha msisitizo kwa mabeki hao wa pembeni ambapo kuna
kipindi alililazimika kuwa mkali pale wachezaji hao waliposhindwa kufanyika kiufasaha
hali iliyoonyesha amedhamiria kupata pointi tatu katika mchezo unatakaochezwa
Jumapili ijayo.
Katika
kuonesha msisisizo kocha Omog alikuwa anaonesha kwa vitendo kile alichohitaji
kufanyika na kumfanya kugongana kwa bahati mbaya na mshambuliaji wake Okwi na
kuumia kwenye jicho na kupewa huduma ya kwanza na daktari Yassin Gembe.
Mchezo
uliopita Simba ilitoka suluhu na na Azam FC uliochezwa Jumamosi iliyopita hali iliyomfanya Omog kubadili
mfumo kwani washambuliaji walionekana kuwa butu
Kocha Omog alikigawa
kikosi chake katika makundi mawili, kikosi cha kwanza kiliundwa na Aishi
Manula, Ally Shomari, Mohammed Hussein, Juuko Murshid, Salim Mbonde, James
Kotei, Shiza Kichuya, Said Ndemla, John Bocco, Emanuel Okwi na Mohammed
Ibrahim.
Kikosi cha
pili kilikuwa na kipa Emmanuel Mseja, Muharam Mohammed ambaye ni kocha wa
makipa, Jamal Mwambeleko, Jonas Mkude, Yusuph Mpilipili, Mzamiru Yassin, Jamal
Mnyate, Mwinyi Kazimoto, Laudit Mavugo na Nicholas Gyan.
Katika
mazoezi hayo kikosi A kilishinda mabao 2-1 yaliyofungwa na Okwi na Bocco na
kikosi B lilifungwa na Gyan.
No comments:
Post a Comment