Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, September 6, 2017

KATIBU MKUU WA TASWA AMIR MHANDO ATEULIWA KATIBU WA KAMATI TUZO TFF



 Image result for AMIR MHANDO
MHARIRI wa SpotiLeo Amir Mhando ametuliwa kuwa Katibu wa Kamati ya tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na mwandishi mwandamizi wa michezo wa HabariLeo Zena Chande mjumbe.
Wawili hawa ambao ni wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN)  wanaungana watu wengine tisa katika kamati hiyo
Akizungumza na wandishi wa habari leo Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema Rais Wallace Karia ametua kamati hiyo ambayo itakuwa na kazi ya kukutana kila mwisho wa mwezi kuchagua mchezaji bora wa ligi kuu.
“Mwenyekiti ni Ahmed Msafiri Mgoyi, Makamu Mwenyekiti ni Almas Kasongo na Katibu ni Amir Mhando,” alisema Lucas.
Wajumbe ni  Zena Chande, Patrick Kahemele, Kennedy Mwaisabula, Said George, Saleh Ally, Ibrahim Masoud, Fatuma Likwata na Gift Macha.
Lucas alisema kamati hii itakuwa na kazi ya kuangalia magoli yanayofungwa kwa ajili ya kushindanishwa katika tuzo za msimu

No comments:

Post a Comment