WASANII wa
bongo muvi wameomba Watanzania kununua kama zao kwani wamejua walipokosea na
sasa wamejirekebisha.
Hayo
yalisemwa jana na Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere wakati wa kuzindua
kampeni ya Uzalendo Kwanza ambayo itafanyika nchi nzima.
Steve
alisema kampeni hiyo ni maalumu kuumunga mkono Rais wa Jamhuri wa Tanzania,
John Magufuli ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhimiza uzalendo ikiwa ni pamoja
na kulipa kodi kwa kudai risiti unapofanya malipo.
“Kampeni ya
Uzalendo Kwanza itazunguka nchi nzima kwa ajili ya kuahamasisha Watanzania wote
kuipenda nchi yao na kutunza raslimali zilizopo ikiwa ni pamoja na kununua kazi
zinazozalishwa na Watanzania wenyewe,”
“Sisi wasanii
wa filamu tunawaomba Watanzania wanunue kazi zetu kwani tumejua tulipokosea na
tumebadilika na kwa kufanya hivyo tunasaidia kuingiza kipato kwa nchi kwani
tunalipa kodi kupitia stampu iliyopo kwenye kasha,” alisema Steve.
Pia alisema
Tanzania inawadai hivyo ni muhimu wakaunangisha nguvu kulinda Amani na kulinda
raslimali za nchi na kuahidi kutoa kazi nzuri.
Naye msanii
mkongwe Bibi Mwenda aliwaasa wazazi kuwafundisha watoto kuwa wazaqlendo kwani
wamezaliwa Tanzania na Tanzania ndio nchi yao.
“Utamsikia
mtoto anasema Bongo bahati mbaya na wewe mzazi unanyamaza, hiyo haipendezi,
Tanzania ni nchi yetu lazima tuipende,” alisema Bibi Mwenda
No comments:
Post a Comment