ALIYEKUWA
kocha Mkuu wa Njombe Mji, Hassan Banyai amesema mashabiki wa timu hiyo
walimtishia maisha ndio maana alilazimika kujiuzulu baada mchezo dhidi ya Mbeya
City.
Akizungumza
na wandishi wa habari Dar es Salaam Banyai alisema baada ya mchezo
kumalizika kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya mashabiki hao walianza kumzonga
Makamu Mwenyekiti Emanuel Mbeyela na
kuanza kutoa vitisho
“Baada ya
kumaliza mchezo mashabiki walifanya kitendo ambacho siyo cha kiungwana cha
kumfuata na kumzunguka Mwenyekiti wa timu Erasto Mpete na Makamu Mwenyekiti Emanuel
Mbeyela baadae walinifuata kambini wakanikuta niko na wachezaji lakini
hawakunidhuru,”
“Wakaniambia
hii timu ni yetu na viongozi sisi ndio tumewaweka, tunakuomba kwa usalama wako
usirudi Njombe ukiwa na timu maana tutakufanya chochote. Nilitafakari kwa kina
na viongozi wakanipigia simu wakaniambia niondoke kambini maana siyo salama
kwangu,” alisema Banyai.
Banyai
alisema alilazimika kuhama hoteli aliyokuwa awali kwa ajili ya usalama wake na
baadae akawasiliana Mpete na kumweleza azma yake ya kujiuzulu na kumkubalia na
kumweleza kwa usalama wa maisha yake na familia ni bora akajiuzulu.
Lakini
Banyai hakuishia hapo alisema baadhi ya viongozi wanamtupia lawama timu kufanya
vibaya jambo ambalo anadai uongozi ndio wenye tatzo kwa sababu wakati timu
inapanda ligi kuu alikabidhi ripoti lakini ripoti hiyo haikufanyiwa kazi.
“Niliikuta
Njombe Mji ikiwa nafasi ya nne kwenye ligi daraja la kwanza lakini
nilibadilisha timu na hatimaye ikapanda daraja, baada ya kupanda nilipendekeza
namna nafasi za kufanyia usajili, kambi, vifaa, uwanja wa mazoezi na mechi za
majaribio tano lakini kati ya vyote nilipata mechi za majaribio tu,”
Nilifika
mahali nikachukua beeps zangu na kocha msaidizi akaleta zake na nililazimika kufanya
mazoezi mara moja kwa siku kwa sababu uongozi ulisema hauna pesa na usajili
wakafanya wanavyojua wao lakini baada nililazimika dakika za mwisho
nililazimika kuongeza Ditrim Nchimbi, Awadh Juma na wengine wawili,” alisema
Banyai
Banyai
anasema sehemu waliyoweka kambi wakati wa maandalizi haikuwa rafiki kwa
wachezaji kwani ilikuwa na mwingiliano mkubwa wa watu na kuzungukwa na kumbi za
starehe jambo ambalo ni gumu kuwadhibiti wachezaji ukizingatia wachezaji
wanapendwa na wanawake.
Pamoja na
yote alishukuru uongozi wa timu hiyo kwani wamemlipa stahili zake zote na
kuwatakia kila la heri katika ligi kuu.
No comments:
Post a Comment