UONGOZI wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), umeomba radhi wanafamilia wote wa
mpira wa miguu kutokana na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho
wa Ngao ya Jamii iliyotolewa juzi
Ngao hiyo
ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha Simba na Yanga za Dar es Salaam
kwenye Uwanja wa Taifa ambapo Simba ilishinda kwa penalti 5-4 na kutwaa Ngao
hiyo.
Ngao hiyo
ambayo ilitengenezwa kwa mbao iliandikwa Community Sheild badala ya Community
Shield neno ambalo lilipoteza maana ya neno Ngao ya jamii na wadau wengine
wakihoji kwanini hawakutumia lugha adhimu ya Kiswahili
Akizungumza
na gazeti hili, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema Watanzania hususani
wanafamilia ya soka TFF haijapokea vizuri muonekana wenye makosa kwenye Ngao ya
Jamii kama ambavyo wadau hawajapokea vema suala hili.
“Kutokana na
makosa hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, tayari amechukua hatua za kinidhamu kwa
watumishi waliohusika na amewasiliana na uongozi wa Simba kuirejesha Ngao hiyo
ili kufanyiwa marekebisho yatakayobaki kwenye kumbukumbu sahihi,” alisema Lucas
Pia Lucas
alisema hawategemei tukio kama hili kujirudia tena.
Hii ni mara
ya pili Ngao ya Jamii inayotolewa na TFF kuwa na makosa kwani msimu wa
2016-2017 Azam FC baada ya kuifunga Yanga ilipewa Ngao ambayo ilibanduka
maandishi yaliyobandikwa kwani ilikuwa ya kioo.
No comments:
Post a Comment