SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa
Kamati ya Utendaji, limeongeza idadi ya timu shiriki kwenye Ligi Kuu Bara msimu
ujao 2018/19 kutoka 16 hadi 20 ili kuongeza ushindani zaidi katika ligi.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema
uamuzi huo umepitishwa jana na Kamati ya Utendaji ya TFF iliyofanyia
marekebisho Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza inayoanza Septemba 16, mwaka huu.
Alisema kutokana na marekebisho hayo, timu
zitakazoshuka daraja mwishoni mwa msimu huu kutoka Ligi Kuu ni mbili hivyo
kubaki 14 ili kuzifanya nne zitakazopanda ziungane na mbili kufanya ziwe 20.
“Kwa mujibu wa utaratibu wa Ligi Daraja la
Kwanza, ina maana msimu huu timu mbili zitapanda kutoka katika kila kundi katika
ligi hiyo ambayo inatarajiwa kuanza Septemba 16, mwaka huu,” alisema Lucas.
No comments:
Post a Comment