Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 26, 2017

MAYANGA ATAJA KIKOSI, YONDANI NDANI BAADA YA KUKAA NJE KWA MWAKA





BEKI wa Kati wa Yanga, Kelvin Yondani amerejea kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kilichotajwa jana na kocha Salum Mayanga kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA.
Yondani ndio mara ya kwanza kuingia kwenye kikosi cha Mayanga kwani mara ya mwisho kuitwa ni Septemba 2016 wakati Taifa Stars ikifundishwa na kocha Charles Mkwasa.
Akizungumza na wandishi wa habari Kocha mkua wa Taifa Stars, Salum Mayanga alisema amewaita wachezaji 21 kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Botswana ambayo inatarajiwa kuchezwa Septemba 2 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mayanga alisema kabla ya kuita wachezaji anawasiliana na mchezaji na daktari wa timu anayocheza ili kujua afya yake na alipokabidhiwa mikoba Yondani aliomba asiwekwe kwenye timu hiyo kwa sababu alikuwa kwenye maadalizi ya ndoa yake na sasa amesema yupo tayari kuitumikia timu ya Taifa baada ya kumaliza mambo yake ya ndoa
 “Wakati nakabidhiwa timu nilizungumza na wachezaji wote waliowahi kuwa kwenye timu ya Taifa na Yondani aliniomba nisimjumuishe kwa kuwa alikuwa  kwenye maandalizi ya ndoa baada ya kumaliza nimefanya mawasiliano naye amesema yupo tayari kuitumikia timu ya Taifa”,  alisema Mayanga.
Mara ya mwisho Yondani aliitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ambacho kilikuwa kikijiandaa kwa mechi ya marudiano ugenini dhidi ya Nigeria kuwania kucheza fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) 2017 lakini hakusafiri na timu kwa sababu zilizotajwa ni za kifamilia
Wachezaji wengine walioitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars ni magolikipa; Aishi Manula (Simba), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Yanga)
Mabeki; Gardiel Michael na Kelvin Yondan (Yanga), Boniface Mganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini), Salim Mbonde na Erasto Nyoni (Simba).
Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdalla (Sony Sugar, Kenya), Muzamiru Yassin, Said Ndemla na Shiza Kichuya (Simba), Simon Msuva (Difaa Hassan El- Jadida, Morocco), Farid Mussa (Tenerrife B, Hispania) na Ergenes Mollel. (Ureno).
Washambuliaji ni Raphael Daud, (Yanga) Kelvin Sabato, (Mtibwa Sugar) (KRC Genk, Ubelgiji) na Elius Maguli (Dhofar FC, Oman).
Pia Mayanga alisema makipa Said Mohammed ‘Nduda’ na Beno Kakolanya na mshambuliaji John Raphael Bocco, hajawaita sababu ya majeruhi badala yake amemrejesha kipa Mwadini Ali.

No comments:

Post a Comment