Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 22, 2017

JOSE MOURINHO ATAMANI KUKAA OLD TRAFFORD MIAKA 15


José Mourinho anataka abakie kama Meneja wa Manchester United kwa Miaka 15 ingawa amekiri presha ya kazi hiyo inafanya hilo kuwa gumu mno.
Hivi sasa Mourinho ndio ataingia Msimu wa Pili na Man United baada kutwaa Ngao ya Jamii, EFL CUP na UEFA EUROPA LIGI katika Msimu wake wa kwanza na kuirejesha Timu kwenye Mashindano makubwa ya Ulaya UEFA CHAMPIONS LIGI.

Lengo la Mourinho Msimu huu Mpya wa 2017/18 wanaoanza Agosti 13 ni kuwemo mbio za Ubingwa wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, baada ya Msimu uliopita kumaliza Nafasi ya 6.

Mourinho hajawahi kudumu kwenye Klabu moja kwa muda mrefu ukiondoa pale alipoingia Msimu wake wa 4 akiwa na Chelsea Mwaka 2007/08 lakini huko Man United amedokeza anataka kukaa muda mrefu zaidi.
Akiongea na ESPN huko USA ambako Man United wako Ziarani, Mourinho alieleza: “Nipo tayari kwa hili. Nipo tayari kukaa Miaka 15. Nakiri ni ngumu sana kwa sababu ya presha ya kazi yetu na maneno ya Watu wengine wakidai lazima tushinde lakini ukweli ni kuwa ni Mmoja tu anaeshinda! Kila Mwaka mambo huwa magumu zaidi!”
Akimgusia Sir Alex Ferguson ambae alikuwa Meneja wa Man United kuanzia Novemba 1986 hadi Mei 2013 alipostaafu, Mourinho alieleza: “Kwa Klabu hii, kwa Miaka mingi ilikuwa Sir Alex. Watu walizoea hali hiyo. Watu walielewa umadhubuti wa Timu. Baada ya David Moyes na Louis van Gaal, sasa naingia Msimu wangu wa Pili na natumai nitabaki na kuleta umadhubuti ule. Nitajaribu!”

Lakini Mourinho anajua fika sulubu na hatari za Umeneja katika zama hizi baada ya kutimuliwa huko Chelsea Desemba 2015 mara tu baada ya kuwapa Ubingwa Msimu uliopita.

Mourinho amenena: “Unapata mafaikio makubwa Msimu mmoja na wa pili unafeli, unafukuzwa. Ilinitokea Chelsea, imemtokea Claudio Ranieri kule Leicester City na itatokea kwa wengi zaidi. Siku hizi Watu wanaangalia mafanikio ya muda mfupi tu!”

Aliongeza: “Nadhani zama za Sir Alex zilikuwa hazina mfano. Sidhani kama kuna Mtu atafikia mafanikio yake. Hakuna Mtu atakaedumu Klabu moja kwa muda mrefu ule na kuleta mafanikio yale. Nadhani zama za Wenger kule Arsenal zitakuwa ni mwisho wa Meneja kubaki Klabu moja kwa muda mrefu. Mimi nitakachofanya ni kujaribu kustahili kuwepo kwenye Klabu hii kwa sababu sasa kitu kikuu ni mafanikio tu. Ukifanikiwa, unabaki Klabuni, Huna Mafanikio, Hubaki Klabuni!”