MABINGWA wa
Ligi Kuu ya soka Tanzania bara,Yanga wametinga nusu fainali ya Kombe la
SportPesa baada ya kushinda kwa penalti 4-2 dhidi ya mabingwa wa Kenya, Tusker.
Wakati Yanga
wakishinda, watani wao, Simba watamenyana na Nakuru All Stars ya Kenya kesho
katika mechi nyingine ya michuano hiyo. Mchezo wa Yanga ulifanyika katika
Uwanja wa Uhuru na hadi dakika ya 90 zilikuwa suluhu.
Kwa matokeo
hayo, Yanga itacheza nusu fainali na AFC Leopards ya Kenya keshokutwa. AFC
Leopards iliitoa Singida United kwa penalti 5-4.
Kila timu
iliyoingia nusu fainali imejinyakulia dola za Marekani 5,000 sawa na sh milioni
10. Waliofunga penalti za Yanga ni Nadir Haroub 'Canavaro', Obrey Chirwa, Maka
Mwakaluka na Said Mussa. Kipa Deogratius Munishi alipangua penalti ya Clifford
Alwanga.
Naye Stephen
Owusu alipiga mpira juu ukagonga mwamba na kutoka. Walioifungia Tusker ni Noah
Wafula na Brian Osumbe. Timu zote zilishambuliana kwa zamu. Yanga ilijaza
vijana wengi wenye umri chini ya miaka 20.
Yanga: Deogratius Munishi, Nadir Haroub, Juma Abdul, Mohammed Nassor, Andrew Vincent, Pato Ngonyani, Yusuf Mhilu/Bakari Athumani, Maka Mwakalumwa, Obrey Chirwa, Juma Mahadhi/Samwel Greyson dk 90, Emmanuel Martin/Said Mussa dk 61.
Tusker:
Ochenge Duncan, Collins Shivanchi, Martin Kiiza, Lloyd Wahome, James Situma,
Ndawula Moses/ Noah Wafula dk 57, Antony Ndula/Brian Osumba dk 90, Humphrey
Mieno, Michael Khamati/ Clifford Alwanga dk57, Allan Wanga na Abdul Hassan.
Singida
United ilitolewa na AFC Leopards kwa penalti 5-4 baada ya kwenda sare 1-1 hadi
dakika ya 90.
Singida
United ilifunga katika dakika ya 10 kupitia Tafadzwa Kutinyu kwa kichwa baada
ya kupokea mpira wa kona wa Simbarashe Nhivi.
AFC Leopards
walisawazisha dakika ya 63 kupitia kwa Vincent Oburu. Kutokana na mechi hizo
kuwa za mtoano, ilibidi penalti zipigwe.
Salum
Chuku alikosa penalti ya Singida United
kwa kupaisha. Waliopata ni Atupele Green, Hamis Shango, Simbarashe na Muroiwa
Elisha.
Wachezaji wa
AFC Leopards, Mangoli Bernard, Marselas Ingots, Allan Katerega, Otieno Duncan
na Gilbert Fiamengo wote walifunga.
Timu
zilishambuliana kwa zamu na hadi mapumziko, Singida ilikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili AFC Leopards walitawala mpira kwa asilimia kubwa huku Singida
United ikionekana kuchoka mapema, wakasawazisha.
AFC Leopards
inayofundishwa na Kocha Mtanzania, Denis Kitambi itacheza nusu fainali Ijumaa
na Yanga.
Singida
United: Elisha Muroiwa, Said Lubawa, Roland Msonjo, Hassan
Dumba, Salum Chuku, Salum Ally, Wisdom Mtasa/Nizar Khalifan dk. 73,
Tafadzwa Kutinyu, Atupele Green na Simbarashe Nhivi, Shango Hamis.
AFC
Leopards: Andika Gabriel, Sikhai Dennis, Marcus Abwao, Salum Andallah, Ottieno
Duncan, Whyvonne Isuza, Bernard Mangoli, Mawira Joshua, Gilbert Fiamenyo,
Nyakha Haron/Allan Katerega dk 90 na Oburu Vincent/Marselas Ingots dk 90.
No comments:
Post a Comment